ISO 8601 - Wikipedia, kamusi elezo huru
Nenda kwa yaliyomo
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ufafanuzi wa ISO 8601 - upanuzi wote tatu umeonyeshwa ni halali.
ISO 8601
ni mfumo wa kimataifa uliokubaliwa kwa maelewano juu ya namna ya kutaja tarehe na wakati.
Kimetolewa na
Shirika la Kimataifa la Usanifishaji
(kwa
Kiingereza
"International Organization for Standardization (ISO)").
ISO 8601 ni orodha ya mapendekezo namna ya kuandika tarehe na wakati katika mawasiliano ya kimataifa. Jina la kiingereza ni "Data elements and interchange formats -- Information interchange -- Representation of dates and times"
Tarehe
hariri
hariri chanzo
Pendekezo la kutaja tarehe ni muundo wa
YYYY-MM-DD
ambako
ni
mwaka
(year),
ni
mwezi
na
ni
siku
("day"). Hivyo inapendekezwa kutaja tarehe 7 mwezi wa nane mwaka 2007 kama 2007-08-07 na kutosahau sifuri kama mwezi au siku ina
tarakimu
moja tu.
Wakati
hariri
hariri chanzo
Pendekezo la kutaja wakati ni muundo wa kutumia saa 24 kwa siku na kuandika
hh:mm:ss
ambako
ni
saa
(hour),
ni
dakika
na
ni
sekonde
. Hivyo inapendekezwa kutaja wakati wa saa tatu ya asubuhi na dakika thelathini na sita na sekonde 47 kama 09:36:47. Hivyo 23:59:59 ni sekonde moja kabla ya saa sita usiku.
Saa sita usiku kamili unaweza kuandikwa kwa namna mbili kama 00:00 na 24:00 ingawa ni wakati huohuo. Tofauti yake ni nikitaka kutaja mwisho wa siku naweza kuandika: Muda unakwisha leo kwenye saa 24:00. Nikitaka kutaja mwanzo wa siku naweza kuandika: Nafasi inafunguliwa kuanzia kesho saa 00:00.
Juma
hariri
hariri chanzo
Juma
zahesabiwa katika kila mwaka kuanzia 1 hadi 52 au 53. Kwa sababu juma halianzi pamoja na mwaka mpya azimio ni ya kwamba juma ile lenye Alhamisi ya kwanza katika mwaka mpya itakuwa "juma no. 1". Itakuwa pia juma yenye tarehe 4 Januari ndani yake.
Hesabu ya wiki hutumiwa hasa kiuchumi wakati wa kupanga kazi ofisini au kiwandani na wakati wa kupatana huduma kati ya makampuni kama tarehe inaruhusiwa kubadilika kidogo lakini juma ya kutolewa kwa huduma au bidhaa ni muhimu.
ISO 8601 yapendekeza pia kuhesabu
Jumatatu
kama siku ya kwanza katika wiki yaani siku ya kwanza ya kazi kamili baada ya
wikendi
ya kimagharibi. Pendekezo hili halilingani na mapokeo na historia ya juma yenyewe na mafundisho ya kidini hivyo haliangaliwi mahali pengi au kutumiwa pamoja na hesabu ya kiutamaduni ya siku zinazoanza juma kwa
Jumapili
Marejeo
hariri
hariri chanzo
A summary of the international standard date and time notation, by Markus Kuhn
, tovuti ya Department of Computer Science and Technology, Chuo Kikuu cha Cambridge, Uingereza, iliangaliwa Oktoba 2017
Ufafanuzi wa istilahi za ISO 8601
, tovuti ya iso.org
The Mathematics of the ISO 8601 Calendar
, tovuti ya staff.science.uu.nl, iliangaliwa Oktob 2017
Rudishwa kutoka "
Jamii
Vipimo vya wakati
Wakati
ISO 8601
Weka mada
US