Meksiko - Wikipedia, kamusi elezo huru
Nenda kwa yaliyomo
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muungano wa Madola ya Meksiko
Estados Unidos Mexicanos
(Kihispania)
Bendera
Nembo
Wimbo wa taifa:
Himno Nacional Mexicano
"Wimbo wa Taifa wa Meksiko"
Mahali pa Meksiko
Mji mkuu
na mkubwa
Mexico (mji)
Lugha rasmi
Kihispania
Lugha za kikabila
68 lugha za asili
Rais
Claudia Sheinbaum
Rais
wa
Seneti
Gerardo Fernández Noroña
Historia
Mwanzo wa Vita ya Uhuru
16 Septemba 1810
Tangazo la Uhuru
27 Septemba 1821
Katiba ya sasa
5 Februari 1917
Eneo
Jumla
km
1,972,550
(ya
13)
Maji (asilimia)
1.58%
Idadi ya watu
Kadirio la 2025
131,946,900
Msongamano
61/km
PLT
PPP
Kadirio la 2025
Jumla
$3.408 trilioni
Kwa kila mtu
$25,557
PLT
Kawaida
Kadirio la 2025
Jumla
$1.818 trilioni
ya 12
Kwa kila mtu
$13,630
HDI
(2023)
0.789
kati
Gini
(2022)
40.2
Sarafu
Peso ya Meksiko
(MXN)
Majira ya saa
UTC
UTC−8 hadi −5
UTC−7 hadi −5 (DST)
Upande wa magari
Kushoto
Msimbo wa simu
+52
Jina la kikoa
.mx
Meksiko
, rasmi
Muungano wa Madola ya Meksiko'
(kwa
Kihispania
Los Estados Unidos Mexicanos
), ni
nchi
katika
Amerika ya Kaskazini
. Inapakana na
Marekani
upande wa kaskazini,
Guatemala
na
Belize
upande wa kusini,
Bahari ya Karibi
upande wa mashariki, na
Bahari ya Pasifiki
upande wa magharibi. Meksiko ina eneo la takriban kilomita za mraba 1,964,375, na ni miongoni mwa nchi kubwa zaidi
duniani
. Ina mandhari mbalimbali kuanzia jangwa la Chihuahua hadi misitu ya mvua ya Yucatán, na historia tajiri inayojumuisha
ustaarabu
wa kale kama
Wamaya
na
Waazteki
Ina idadi ya watu inayokadiriwa kuwa zaidi ya milioni 126 (2024), na hivyo kuwa nchi ya 10 kwa idadi ya watu duniani. Mji mkuu na mji mkubwa zaidi wa
mji wa Meksiko
ni Mexico City, ambao pia ni kitovu cha
siasa
uchumi
, na
utamaduni
wa
taifa
hilo. Licha ya changamoto kama ukosefu wa usawa wa
kijamii
na usalama, Meksiko ni moja ya nchi zenye
uchumi
mkubwa barani
Amerika
, na ni mwanachama wa mashirika muhimu kama
Umoja wa Mataifa
G20
, na Jumuiya ya Nchi za Amerika (OAS).
Historia
hariri
hariri chanzo
Nchi jinsi ilivyo leo imeundwa na wakoloni Wa
hispania
walioivamia kuanzia mwaka
1519
na kuvunja
utawala
wa milki za wenyeji kama
Azteki
na
Maya
Kabla ya uvamizi wa Hispania
hariri
hariri chanzo
Watu wa kwanza waliofika huko kutoka kaskazini walikuwa
Waindio
, wajukuu wa wahamiaji walioingia
Amerika
kutoka
Asia ya Kaskazini
. Hakuna uhakika kufika huko kulitokea lini: labda miaka 10,000 iliyopita
Hao Waindio walikuwa
wakulima
hodari sana na
mazao
mbalimbali ambayo leo ni msingi wa
chakula
kote
duniani
yalianzishwa na kupandishwa nao, yakiwa pamoja na
mahindi
mboga
na
nyanya
Kilimo
cha mahindi hukadiriwa kilianzishwa takriban mnamo mwaka
9000 KK
Sanamu ya kichwa ya Kiolmeki
Kilimo kiliweka msingi kwa
vijiji
na
jamii
zilizoshirikiana katika maeneo makubwa.
Miji
ya kwanza inajulikana kuanzia takriban mwaka
1500 KK
Staarabu mbalimbali zilistawi na kukua katika maeneo ya pwani (
Waolmeki
, Wamaya) na katika
nyanda za juu
za Mexico ya kati (
Wazapoteki
Wamixeki
Watolteki
, Waazteki).
Waolmeki
hariri
hariri chanzo
Ustaarabu wa kwanza unaojulikana ulikuwa wa
Waolmeki
baina ya 1500 KK na
400 KK
. Habari zao zinajulikana kutokana na
akiolojia
na mabaki ya miji na
sanaa
yao. Waolmeki walijenga miji wakaacha mifano ya sanaa yenye kiwango cha juu.
Waliishi katika kanda la pwani la Mexiko katika majimbo ya leo ya
Veracruz
na
Tabasco
. Ni watu wa kwanza katika Mexiko wanaojulikana kubuni
mwandiko
na
kalenda
mchezo
wa
mpira
na
ujenzi
wa
piramidi
za
hekalu
. Walikuwa hodari sana kuchonga
sanamu
ya
mawe
, hasa
vichwa
vikubwa vyenye
urefu
WA zaidi ya
mita
3. Walifaulu kuunda sanaa hii bila kujua vifaa vya
metali
Hekalu - piramidi ya Kimaya
Ukurasa kutoka kitabu cha Kimaya - maandishi ya hiroglifi
Sanamu nyingine inayorudirudi ni mtu-jagwaa inayounganisha sehemu ya
maumbile
ya
binadamu
na
jagwa
. Takriban mwaka 400–
300 KK
miji yao iliachwa na wakazi; hakuna uhakika ni nini iliyosababisha mwisho wa ustaarabu huu.
Wamaya
hariri
hariri chanzo
Upande wa
mashariki
wa Waolmeki ustaarabu wa
Wamaya
ulianza tangu takriban mwaka
2000 KK
. Wamaya walikalia
rasi
ya
Yucatan
pamoja na Guatemala na Belize ya leo. Waliishi katika vijiji na miji iliyojitegemea na kugombana kati yao mara kwa mara.
Wamaya walibuni mwandiko wa
hiroglifi
wenye
alama
nyingi kupita maandishi mengine katika
Amerika ya Kale
na kutunga
vitabu
. Waliendeleza pia
hisabati
, wakijua
namba
sifuri
" na kuboresha mfumo wa kalenda.
Walikuwa hodari sana katika
astronomia
yaani
elimu
ya
nyota
. Walipamba miji yao kwa
majengo
makubwa na mazuri na kuwa
wafanyabiashara
hodari. Sanaa yao ilijua
uchongaji
wa mawe na pia
uchoraji
Jamii ya Wamaya ilifikia kiwango cha juu kuanzia mwaka
500 KK
wakati miji mikubwa ya kwanza ilipotokea. Mnamo mwaka
800
BK
jamii za Wamaya katika Yucatan ziliporomoka;
wataalamu
wengi huamini ya kwamba mabadiliko ya
ekolojia
na
halihewa
pamoja na kuchoka kwa
rutuba
ya
ardhi
yalisababisha kutoka kwa watu katika makazi ya awali.
Lakini ustaarabu huu uliona tena kipindi cha kustawi katika maeneo mengine hadi kuja kwa Wahispania. Miji mbalimbali ya Wamaya iliendelea kujitetea dhidi ya wavamizi na
Nojpeten
, mji wa mwisho wa kujitegemea ulitekwa mwaka
1696
tu.
Teotihuacan
hariri
hariri chanzo
Barabara
ya mahekalu na piramidi ya jua mjini Teotihuacan
Teotihuacan
ilikuwa mji mkubwa katika nyanda za juu, karibu na Mexico City ya leo. Kuanzia mwaka
100 KK
hadi takriban
550
BK ilikuwa mji mkubwa wa Amerika, pia moja kati ya miji mikubwa duniani na
kitovu
cha
utamaduni
kilichoathiri staarabu zote za Mexiko.
"Teotihuacan" ilikuwa
jina
la Waazteki kwa mji huu, jina la kienyeji halikuhifadhiwa. Maana ya jina ni "mahali pa kuzaliwa kwa
miungu
". Wakati wa
maendeleo
yake mji ulikuwa na eneo la
kilomita za mraba
30 ukiwa na wakazi angalau 150,000, labda hata 250,000 walioishi humo
Hakuna uhakika ni akina nani waliojenga Teotohuacan. Mji wote ulipangwa kwa kufuata
barabara
mbili zilizoelekea kaskazini-kusini na mashariki-magharibi. Hekalu kubwa na piramidi zinaonyesha umuhimu wa
dini
, na mabaki ya
nyumba
za wakubwa na watu wa kawaida yanaruhusu kupata
picha
ya jamii iliyoishi hapa.
Teotohuacan ilikuwa kitovu cha
biashara
ya misafara ya mbali na pia ya elimu. Ukubwa wa mji unaonyesha kiwango cha juu cha
utawala
na
ushirikiano
kati ya watu wake.
Katika
karne ya 6
BK sehemu kubwa ya majengo iliharibika na kuchomwa. Hakuna uhakika kama hii ilikuwa tokeo la uvamizi kutoka nje au vurugu au
mapinduzi
ndani ya mji. Baada ya maharibio yale mji ulianza kurudi nyuma na idadi ya watu kupungua. Mnamo mwaka
750
BK watu wote waliondoka: ni
maghofu
ya majengo makubwa tu yaliyobaki
Milki ya Azteki
hariri
hariri chanzo
Askari wa Azteki
Kuanzia mwaka 1325 kabila la
Azteki
likaunda mji wa
Tenochtitlan
kwenye kisiwa cha
ziwa la Tezcoco
. Waazteki wakaendelea kuunda milki kubwa lililoeena na kutawala sehmu kubwa ya nyanda za juu za Mexiko. Msingi wa milki yao ilikuwa ushirikiano na mji miwili jirani iliyounda mwungano wa pande tatu lakini Waazteki waliendelea kuwa mshiriki mkuu na mtawala wa Tenochtitlan hatimaye alikuwa mtawala mkuu. Walishambulia maeneo ya miji na makabila jirani na kuwalazimisha kulipa kadi kwao. Kama walikubali kutoa kodi kila mwaka na pia kushiriki katika vita za milki watawala wa kienyeji waliruhusiwa kuendelea na utawala wa ndani. Dini yao iliweka uzito kwa sadaka za binadamu waliochinjwa kwenye mahekalu ya miungu yao. Waliunda mfumo wa mikataba ya vita na milki nyingine ambako walikutana kwa mapigano yaliyo kubaliwa awali kwa shabaha ya kukamata wafungwa wengi iwezekanavyo na kuwatoa kama sadaka kwa miungu hekaluni baadaye.
Uvamizi wa Wahispania
hariri
hariri chanzo
Mwaka 1519 Mhispania
Hernan Cortez
alifika kwenye pwani la Mexiko. Katika miaka iliyofuata alifaulu kuendelea hadi mji wa Tenochtitlan akiongozana na kundi la Wahispania mamia kadhaa. Cortez aliweza kuungana na miji na makabila ya Waindio waliochoka utawala wa Azteki na kumpa askari za usaidizi. Mwaka 1520 waliingia Tenochtitlan kama wageni wa mfalme
Montezuma II
wakaendelea kumkamata lakini baada ya kifo cha mfalme walifukuzwa wakakimbia kwa matatizo katika "usiku wa huzuni" (Kihisp.
noche triste
). Waazteki walidhoofishwa sana kutokana na
epidemia
ya ugonjwa wa
ndui
. Cortez aliweza kukusanya jeshi kubwa la Waindio waliopinga Waazteki akavamia na kuharibu Tenochtitlan mwaka 1521 na kwenye magofu ya mji huu alianzisha mji mpya wa
Mexico City
(Kihisp.
Ciudad de Mexico
).
Ukoloni
hariri
hariri chanzo
Jinsi Bikira Maria alivyomtokea Juan Diego kwenye kilima Tepeyac, Mexico City.
Baada ya Hispania kuteka sehemu kubwa ya nchi mwaka 1521, liliundwa
koloni
la
Hispania Mpya
chini ya makamu wa mfalme.
Bila kujali
ukatili
wa Wahispania,
Waindio
walijiunga haraka na
Kanisa Katoliki
kuhusiana na
njozi
ya mwenzao
Juan Diego
aliyetokewa na
Bikira Maria
huko
Guadalupe
12 Desemba
1531
), wakachanganyikana na wavamizi na kufanya
taifa
jipya lenye sura ya
kichotara
, kiasi kwamba wengi wanajiona "mestizos" (machotara) hata wasipokuwa na
damu
mchanganyiko.
Tangu uhuru hadi leo
hariri
hariri chanzo
Baada ya
karne
tatu na baada ya
vita
vya
ukombozi
, mwaka 1821 wakazi walijipatia
uhuru
kwa jina la Mexico.
Vita ya uhuru
hariri
hariri chanzo
Mfano wa
uhuru wa Marekani
mwaka
1776
ulikuwa na athira pia kati ya wasomi wenyeji wa Mexiko. Jamii ya kikoloni iliundwa juu ya
ubaguzi
kati ya Kreoli (walowezi wenye asili ya Hispania bila mchanganyiko na Waindio), Mestizos (asilimia kubwa ya wenyeji waliotokana na
ndoa
za
wanaume
Wahispania na
wanawake
Waindio) na Waindio wenyewe. Lakini vyeo vyote vya juu, kama maafisa wa juu wa serikali, vilipatikana pekee kwa watu waliozaliwa Hispania na kutumwa Mexiko. Mawazo ya uhuru yalianza kupatikana kati ya Kreoli na Mestizos wa matabaka ya juu.
Chanzo cha vita ya uhuru kilikuwa mabadiliko katika
Ulaya
Napoleon
mtawala wa
Ufaransa
alimkamata mfalme
Ferdinand VII
wa Hispania akamlazimisha kujiuzulu na kumpa
kaka
yake
Yosefu Napoleon
ufalme wa Hispania
. Hatua hii ilifuatwa na wimbi la uasi nchini Hispania dhidi ya mfalme Mfaransa.
Katika Hispania Mpya (Mexico) kamati za miji kadhaa zilizoongozwa na Kreoli ziliapa kumfuata mfalme mfungwa halali pekee. Kamati Kuu ya Mexiko City ilitaka kuanzisha bunge la pekee kwa sababu Hispania haikuwa tena na serikali halali. Mfalme mdogo (gavana mkuu) alikubali. Viongozi wengine walitangaza ilhali mfalme halali hayuko tena sasa, nguvu yote iko mkononi mwa wananchi. Hapo Wahispania katika koloni walioshika vyeo vikuu waliamua kumpindua mfalme mdogo na kuwakamata viongozi wa Kreoli.
Uasi ulifaulu lakini vikundi vidogo vya wapinzani wa uhuru kutoka Hispania waliendelea kukutana nchini na kukusanya viongozi. Hatimaye
padre
Kreoli
Miguel Hidalgo y Costilla
alikusanya jeshi la
wanamgambo
wakulima
Waindio na Kreoli akapigana na jeshi lililokuwa chini ya mamlaka ya maofisa Wahispania. Miguel Hidalgo alishindwa na kuuawa, lakini hii ilikuwa chanzo cha uasi mkubwa ambao Wakreoli na wakulima Waindio walipigana na jeshi lililofuata amri ya Wahispania katika koloni.
Mwaka kiongozi wa upande wa migambo ya uhuru Guerrero na jenerali wa jeshi la serikali
Agustin de Iturbide
walikutana wakapatana kuungana. Vikosi vingi vya jeshi la kikoloni vilihamia upande wao. Gavana mpya aliyefika kutoka Hispania aliamua kukubali uhuru uliotangazwa tarehe
28 Septemba
1821
. Iturbide alikuwa
rais
wa kwanza na baadaye kwa kipindi kifupi
Kaisari
wa Mexiko hadi kujiuzulu mwaka
1823
: hapo Mexiko ikaendelea kuwa
jamhuri
Karne ya 19
hariri
hariri chanzo
Maeneo yaliyoongezwa, yaliyotengwa au kujitenga na Mexiko tangu uhuru wa mwaka 1821: A) Maeneo yaliyotwaliwa na Marekani (nyekundu, kichungwa, nyeupe), Chiapas kuchukuliwa kutoka Guatemala (buluu), eneo la Yucatan lililotwaliwa (nyekundu) na maeneo ya Shirikisho la Amerika ya Kati (
zambarau
).
Katika miaka iliyofuata nchi haikupata msimamo imara kisiasa wala kiuchumi. Serikali mara nyingi zilikuwa hafifu na kubadilishana.
Vikundi vya
ushikiliaji ukale
na
uliberali
vilipigana hadi kuingia katika
vita ya wenyewe kwa wenyewe
Mwaka wa uhuru maeneo ya kusini yalijitenga na kuwa
Shirikisho la Amerika ya Kati
lililofarakana baadaye kuwa nchi za
Guatemala
Honduras
El Salvador
Nikaragua
na
Costa Rica
Mwaka
1835
Marekani ilijaribu kununua maeneo ya
Texas
na
Kalifornia
lakini Meksiko ilikataa. Hata hivyo utawala wa Mexiko kuhusu maeneo haya ya kaskazini yake ulikuwa hafifu na wa juujuu tu, Waindio walijitegemea hali halisi nje ya miji michache. Hivyo serikali ya Mexiko ilikaribisha walowezi kutoka Marekani kuhamia Texas. Hao walowezi wenye utamaduni wa
Kiingereza
-Kimarekani walitangaza uhuru wao mwaka
1836
wakaunda
Jamhuri ya Texas
iliyochukuliwa na Marekani mwaka
1845
kuwa jimbo lake.
Hatua hii ilisababisha
Vita ya Marekani na Mexiko
ya miaka
1846
1848
. Mexiko ikashindwa na kaskazini yote ikawa sehemu ya Marekani (
Kalifornia
New Mexico
Arizona
Nevada
Utah
na
Colorado
, jumla
theluthi
moja ya eneo lake lote.
Mexiko ilishambuliwa mara mbili na
Ufaransa
kutokana na madai juu ya
madeni
ya taifa kwa
raia
au
benki
za nje. Kwenye
vita ya keki
1838
1839
) Ufaransa ilidai fidia kwa uharibifu uliotokea katika duka la keki la Mfaransa mjini Mexiko na
manowari
za Ufaransa zilishambulia bandari za Mexiko hadi rais wake kukubali deni hili.
Mashambulio makubwa zaidi yalifuata mwaka
1861
. Mexiko ilishindwa kulipa madeni kwa mataifa ya nje. Ufaransa chini ya
Napoleon III
iliamua kufanya Mexiko nusu-koloni yake; jeshi la Ufaransa ilivamia nchi, kufukuza serikali na kumweka
Mwaustria
Maximilian I
kama "Kaisari wa Mexiko". Serikali ya rais
Benito Juarez
ilipinga uvamizi huu kwa njia ya vita ya wanamgambo na mwaka
1866
Wafaransa walipaswa kuondoka tena, Maximilian aliuawa mwaka
1867
Karne ya 20
hariri
hariri chanzo
Utawala wa rais
Porfirio Díaz
uliendelea kwa miaka zaidi ya 30 na kuwasha moto ya
mapinduzi ya Mexiko
alipojaribu kushinda tena kwa udanganyifu mwaka
1910
Miaka hadi 1921
vita ya wenyewe kwa wenyewe
iliharibu sehemu kubwa za nchi. Kuna makadirio ya kwamba wananchi milioni 1,5 (kati ya milioni 15) waliuawa na zaidi ya 200,000 walikuwa
wakimbizi
, hasa kwenda Marekani
Mwaka
1917
katiba mpya ya nchi ilitolewa na mkutano wa bunge maalumu. Katiba hii ilikuwa katiba ya kwanza duniani kutangaza
haki za kijamii
. Hizo haki zililenga kutunza na kuboresha hali ya wananchi wenye maisha magumu kama wafanyakazi na wakulima dhidi ya
mabepari
na wenye mashamba makubwa
. Katiba hii iliweka mamlaka nyingi mikononi mwa rais wa taifa anayechaguliwa na wananchi wote kwa kipindi kimoja cha miaka 6, halafu hawezi kuchaguliwa tena. Shabaha nyingine ya vifungu katika katiba ilikuwa kupunguza uwezo wa Kanisa Katoliki kuathiri siasa na jamii na hatimaye kukomesha
imani
hiyo.
Siasa hii dhidi ya
Ukristo
iliendelea chini ya rais Calles na kusababisha kipindi kingine cha vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka ya
1926
1929
. Katika mapigano hayo yaliyoitwa
La Cristiada
wakulima wengi walichukua silaha kwa jina la
Kristo
Mfalme
dhidi ya jeshi la serikali ili kutetea
uhuru wa dini
, wakipinga kufungwa kwa
makanisa
, kuzuiwa
ibada
mbalimbali za hadhara na kuuawa kwa mapadre kama
Mtakatifu
Kristofa Magallanes
na wenzake. Vita hivyo vilisababisha vifo 250,000 na idadi hiyohiyo ya wakimbizi waliojisalimisha Marekani.
Baada ya mapinduzi mamlaka ilichukuliwa na Chama cha kitaifa cha mapinduzi (Partido Nacional Revolucionario PNR) kilichoendelea kutawala kwa miaka 71 kuanzia 1929 hadi
2000
Watu
hariri
hariri chanzo
Wakazi ni 129,875,529: wengi wao ni ma
chotara
wenye
damu
ya
Wahindi wekundu
(31/55% hivi) na
Wazungu
(42/65% hivi). Wenye asili ya
Ulaya
tu ni 9/18%. Wenye asili ya
Afrika
ni 2%.
Ni nchi ya kwanza duniani kwa wingi wa watu wanaotumia
lugha
ya
Kihispania
ambayo ni
lugha ya taifa
, lakini wengine (9.8/14.9%) wanaendelea kutumia lugha asilia tangu kabla ya
ukoloni
kama vile
Nahuatl
Yukatek
Maya
Mixtek
na
Zapotek
Nchini wanaishi Wamarekani milioni 1, halafu
wahamiaji
wengine kutoka Amerika ya Kati,
Lebanon
, nchi nyingine za
Asia
n.k. Kinyume chake, Wameksiko 13 milioni wako Marekani, na raia wengine 23 milioni wa nchi hiyo wana asili ya Meksiko.
Upande wa
dini
walio wengi ni wafuasi wa
Yesu Kristo
katika
Kanisa Katoliki
(77.7%) au
madhehebu
mengine (11.2%). Ni nchi ya pili duniani kwa wingi wa Wakatoliki, baada ya
Brazil
, na karibu
nusu
kati yao wanashiriki
ibada
kila
wiki
. Wasio na dini ni 8.1%.
Majimbo ya Mexiko
hariri
hariri chanzo
Aguascalientes
Baja California
Baja California Sur
Campeche
Chiapas
Chihuahua
Coahuila
Colima
Durango
Guanajuato
Guerrero
Hidalgo
Jalisco
Mexico
Michoacán
Morelos
Nayarit
Nuevo León
Oaxaca
Puebla
Querétaro
Quintana Roo
San Luis Potosí
Sinaloa
Sonora
Tabasco
Tamaulipas
Tlaxcala
Veracruz
Yucatán
Zacatecas
Ramani ya Mexiko
Tazama pia
hariri
hariri chanzo
Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
Orodha ya milima ya Meksiko
Tanbihi
hariri
hariri chanzo
Michael S. Werner (January 2001). Concise Encyclopedia of Mexico. Taylor & Francis. pp. 386–. ISBN 978-1-57958-337-8
A single domestication for maize shown by multilocus microsatellite genotyping, Proc Natl Acad Sci U S A. 2002 Apr 30; 99(9): 6080–6084. doi: 10.1073/pnas.052125199
"The Evolution of Corn". University of Utah HEALTH SCIENCES. Retrieved 2 January 2016"
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2016-04-01
. Iliwekwa mnamo
2016-03-20
"Architecture, Astronomy, and Calendrics in Pre- Columbian Mesoamerica, Vincent H. Malmstrom"
(PDF)
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
(PDF)
mnamo 2006-11-03
. Iliwekwa mnamo
2016-03-21
Teotihuacan, Department of Arts of Africa, Oceania, and the Americas, The Metropolitan Museum of Art October 2001
Ndui ilikuwa ugonjwa iliyokuwa kawaida katika Ulaya wakati ule lakini ilikuwa ugonjwa mgeni kwa wenyeji wa Amerika ambao walikosa kinga dhidi yake; hivyo ilikuwa kati ya magonjwa wa kuambukizwa kutoka Ulaya yaiyoua Waindio wengi katika karne zilizofuata.
Robert McCaa, "Missing millions: the human cost of the Mexican Revolution." Mexican Studies 19#2 (2001)
Akhtar Majeed, Ronald Lampman Watts, and Douglas Mitchell Brown (2006). Distribution of powers and responsibilities in federal countries. McGill-Queen's Press. p. 188. ISBN 0-7735-3004-5.
Marejeo
hariri
hariri chanzo
Camp, Roderic A.
Politics in Mexico: Democratic Consolidation Or Decline?
(Oxford University Press, 2014)
Davis, Diane.
Urban leviathan: Mexico City in the twentieth century
(Temple University Press, 2010)
Domínguez, Jorge I (2004). "The Scholarly Study of Mexican Politics".
Mexican Studies / Estudios Mexicanos
20
(2): 377–410.
Edmonds-Poli, Emily, and David Shirk.
Contemporary Mexican Politics
(Rowman and Littlefield 2009)
Kirkwood, Burton.
The History of Mexico
(Greenwood, 2000)
online edition
Ilihifadhiwa
24 Desemba 2009 kwenye
Wayback Machine
Krauze, Enrique
(1998).
Mexico: Biography of Power: A history of Modern Mexico 1810–1996
. New York: Harper Perennial. uk.
896.
ISBN
0-06-092917-0
Meyer, Michael C.; Beezley, William H., whr. (2000).
The Oxford History of Mexico
. Oxford University Press. uk.
736
ISBN
0-19-511228-8
Levy, Santiago.
Good intentions, bad outcomes: Social policy, informality, and economic growth in Mexico
(Brookings Institution Press, 2010)
Meyer, Michael C., William L. Sherman, and Susan M. Deeds.
The Course of Mexican History
(7th ed. Oxford U.P., 2002)
online edition
Ilihifadhiwa
2 Februari 2011 kwenye
Wayback Machine
Russell, Philip (2010).
The history of Mexico: from pre-conquest to present
Routledge
ISBN
978-0-415-87237-9
. Iliwekwa mnamo
Julai 9,
2010
{{
cite book
}}
: CS1 maint: date auto-translated (
link
Tannenbaum, Frank.
Mexico: the struggle for peace and bread
(2013)
Werner, Michael S. ed.
Encyclopedia of Mexico: History, Society & Culture
(2 vol 1997) 1440pp
online edition
Ilihifadhiwa
24 Januari 2010 kwenye
Wayback Machine
Werner, Michael S. ed.
Concise Encyclopedia of Mexico
(2001) 850pp; a selection of unrevised articles
Viungo vya nje
hariri
hariri chanzo
The Presidency of Mexico
Mexico Tourism Official Website | VisitMexico
Ilihifadhiwa
4 Juni 2012 kwenye
Wayback Machine
Mexico
entry at
The World Factbook
Mexico
Ilihifadhiwa
7 Juni 2008 kwenye
Wayback Machine
from
UCB Libraries GovPubs
Meksiko
katika Open Directory Project
Mexico
from the
BBC News
Mexico
at
Encyclopædia Britannica
Wikimedia Atlas of Mexico
Key Development Forecasts for Mexico
from
International Futures
Mexico by World Painters.
Rudishwa kutoka "
Jamii
Mexiko
Nchi zinazotumia Kihispania
Amerika ya Kaskazini
Nchi za G20
Jamii zilizofichwa:
Kurasa zinazotumia marudio ya hoja katika wito wa kigezo
CS1 maint: date auto-translated
Meksiko
Weka mada
US