Ukristo - Wikipedia, kamusi elezo huru
Nenda kwa yaliyomo
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ukristo
Χριστιανισμός
Msalaba wa Kikristo
Uainishaji
Dini ya Abrahamu
Maandiko
Biblia ya Kikristo
Agano la Kale
na
Agano Jipya
Teolojia
Mungu mmoja tu
katika
Utatu
wa
nafsi
Eneo
Dunia
karibu nzima
Lugha
Kiebrania
Kiaramu
Kigiriki
na nyingine zote
Mwaasisi
Yesu
Kristo
Asili
Karne ya 1
BK
Yudea
Dola la Roma
Ibada
Sala
Ubatizo
Ekaristi
n.k.
Wafuasi
Bilioni 2.4
onesha
uthibitisho
Sanamu ya Kristo mkombozi
huko
Rio de Janeiro
Brazil
) ni
sanamu
ya
Yesu
kubwa kuliko zote zilizopata kutengenezwa.
Ukristo
(kutoka neno la
Kigiriki
Χριστός, Khristos, ambalo linatafsiri lile la
Kiebrania
מָשִׁיחַ, Māšîăḥ, linalomaanisha "Mpakwamafuta"
) ni
dini
inayomwamini
Mungu
pekee
kama alivyofunuliwa kwa
Waisraeli
katika
historia ya wokovu
ya
Agano la Kale
na hasa
Yesu Kristo
katika
Agano Jipya
ambaye ni
mwanzilishi
wake katika
karne ya 1
Dini hiyo, iliyotokana na ile ya
Wayahudi
, inalenga kuenea kwa
binadamu
wote, na kwa sasa ni
kubwa
kuliko zote
duniani
ikiwa na wafuasi 2,400,000,000 (33% kati ya watu 7.274 bilioni)
, ambao
nusu
ni waamini wa
Kanisa Katoliki
na nusu ya pili wamegawanyika kati ya
Waorthodoksi
(11.9%) na
Waprotestanti
(38%) wa
madhehebu
mengi sana.
Karibu wote wanakubali
Utatu Mtakatifu
, yaani kwamba
milele
yote Mungu ni
nafsi
tatu
zenye
umoja
kamili:
Baba
Mwana
na
Roho Mtakatifu
. Ni kwa
jina
lao kwamba
mataifa
yote wanahimizwa kubatizwa kwa
maji
, ili kuzaliwa upya, kadiri ya agizo la Yesu ili kuingizwa katika
fumbo
la Mungu pekee kupitia fumbo la kifo na ufufuko wake mwenyewe.
Kitabu
kitakatifu cha Ukristo kinajulikana kama
Biblia
. Ndani yake inategemea hasa
Injili
na vitabu vingine vya
Agano Jipya
Wakati wa
Mababu wa Kanisa
misingi ya
imani
ya Ukristo ilifafanuliwa na
Mitaguso ya kiekumeni
namna inayokubaliwa na wengi kabisa kati ya Wakristo wa leo.
Maungamo yao
yanakiri kwamba Yesu ni
Mwana wa Mungu
aliyefanyika mtu ili kuwaokoa
binadamu
. Baada ya kuteswa na kuuawa
msalabani
alizikwa ila
akafufuka
, siku ya tatu akapaa kwa Mungu akishiriki
mamlaka
ya Baba hadi
atakaporudi
kuhukumu waadilifu na wasiotubu
, akiwapa
tuzo
au
adhabu
ya
milele
kadiri ya imani na matendo yao.
Hivyo, kati ya
madhehebu
ya Ukristo, karibu yote yanamkiri
Yesu
kuwa kwa pamoja Mungu kweli na mtu kweli: katika
umoja
na
nafsi
yake ya Kimungu zinapatikana sasa hali hizo zote mbili.
Yote yanamkiri kuwa
Mwokozi
wa watu wote, na kuwa ndiye atakayerudi mwishoni mwa
dunia
kwa
hukumu
ya wote, ingawa maelezo kuhusu jambo hilo yanatofautiana.
Vilevile yote yanamchukua kama
kielelezo
cha
utakatifu
ambacho - kwa msaada wa
Roho Mtakatifu
na wa
sakramenti
zilizowekwa na Yesu mwenyewe, kuanzia ile ya
ubatizo
- kiwaongoze ndani ya
Kanisa
katika
maadili
yao maalumu, kuanzia
unyenyekevu
na
upole
hadi
upendo
unaowaenea wote, bila kumbagua yeyote, hata
adui
Asili
Chimbuko la Ukristo ni mtu huyo aliyezaliwa takriban miaka 2000 iliyopita huko
Mashariki ya Kati
, katika
kijiji
cha
Bethlehemu
kilichopo hadi hivi leo kwenye mipaka ya
Palestina
; alikuwa akiitwa
Yesu
wa
Nazareti
kijiji
alikokulia) au
mwana
wa
Yosefu
mchonga samani
mama
yake akifahamika kwa
jina
la
Bikira Maria
Kwa kumuita pia
Kristo
, wafuasi wake walikiri kwamba ndiye aliyetimiza
utabiri
wa ma
nabii
wa kale, kama unavyopatikana katika
vitabu
vya
Biblia ya Kiebrania
na
Deuterokanoni
Habari za maisha na mafundisho yake zinapatikana kirefu zaidi katika
Injili
nne zilizokubalika, katika
Agano Jipya
kwa jumla, lakini pia ziliandaliwa na kutabiriwa na
Agano la Kale
Yesu kama Masiya aliyetarajiwa
Ukristo ni matokeo ya
utume
wa Yesu, uliopokewa na waliomwamini kuwa ndiye
Masiya
, yaani
mkombozi
aliyetimiliza ahadi za Mungu kwa
binadamu
Katika
kitabu cha Mwanzo
tunasoma
utabiri
wa kuja kwake ulianzia katika
bustani
ya
Edeni
pale Mungu alipomwambia
nyoka
, yaani
shetani
, kuhusu
mwanamke
kwamba "uzao wake utakuponda kichwa" (
Mwa
3:15).
Baadaye
Abrahamu
, babu wa
taifa
la
Israeli
, kwa
imani
na
utiifu
wake kwa Mungu, aliahidiwa kwamba katika
uzao
wake mataifa yote
yatabarikiwa
Musa
mwanaharakati
aliyewakomboa watu wa Israeli kutoka
utumwani
Misri
takribani miaka
1250 KK
(kabla ya kuzaliwa kwa Yesu), ndiye
nabii
wa kwanza kutabiri wazi kwa niaba ya Mungu ujio wa Masiya au Kristo (
Kumb
18:15-22, hususan mstari 18: "Nitawainulia nabii kama wewe kutoka miongoni mwa ndugu zenu; na nitatia neno langu kinywani mwake na atasema nao yote niliyomwamuru."
Kuja kwake kulitimia katika Agano Jipya, ambalo ni ukamilifu wa yote yaliyotabiriwa katika
Agano la Kale
. Kwani Musa alitumwa kuanzisha Agano la Kale kama maandalizi ya Agano Jipya, akikabidhi mifumo mingi ya nje na ndani kwa watawala na
waamuzi
waliomfuatia watakaoshikilia Agano la kusubiri Masiya wakishirikiana na ma
nabii
na ma
kuhani
Yesu alizaliwa miaka kama 1800 baada ya Abrahamu. Vitabu vya
Injili
vinaeleza matukio na mafundisho ya Yesu ambayo ndiyo mwongozo wa
imani
hiyo.
Maisha
na
kazi
ya Yesu vimeibua mambo mengi katika
historia
. Ndiyo sababu
kalenda
iliyoenea duniani huhesabu miaka kutoka ujio wake; huu ni
mchango
mmojawapo wa Ukristo katika
ustaarabu
Mafundisho ya msingi ya Yesu
Hotuba ya Mlimani
kadiri ya
Carl Heinrich Bloch
Hotuba ya Mlimani
inachukuliwa na Wakristo kuwa utimilifu wa
Torati
iliyotolewa na
Musa
katika
Mlima Sinai
Yesu alifanya
ishara
za kustaajabisha, au
miujiza
. Matokeo ni kwamba, watu wengi wakamwamini.
Nikodemu
, mshiriki mmojawapo wa
baraza
la
Sanhedrini
, ambalo lilikuwa pia
mahakama kuu
ya Wayahudi, alivutiwa na kutaka kujua zaidi kuhusu
siri
ya miujiza hiyo na
ujumbe
kutoka kwa Mungu; kwani yeye alihamasika kuona ishara zile kutoka kwa Mungu.
Yesu akamjibu kwamba hakika mtu hawezi kuingia
ufalme wa Mungu
asipozaliwa mara ya pili kwa
maji
na
Roho Mtakatifu
Pia akajieleza kuwa
mpatanishi
wa
ulimwengu
wa
dhambi
na Mungu na kwamba kila anayemgeukia kwa
imani
hatapotea, bali atarithi
uzima wa milele
: alisema mwenyewe ni mfano wa
nyoka wa shaba
aliyetengenezwa na Musa. (
Yoh
2:23-3:21;
Hes
21:9).
Akiwa kando ya
Ziwa la Galilaya
, Yesu alikuta
umati
wa watu umekusanyika. Basi akapanda
mashuani
na kuenda mbali kidogo na
ufuoni
, akaanza kuwafundisha kuhusu
Ufalme wa mbinguni
kupitia mfululizo wa
mifano
Mmojawapo ni huu ufuatao: "Ufalme wa mbinguni ni kama punje ya
haradali
ambayo mtu anaipanda. Ingawa ni
mbegu
ndogo sana inakua na kuwa
mti
wa
mboga
mkubwa kuliko yote. Inakuwa mti ambao
ndege
wanauendea, wakipata makao katika matawi yake". (
Math
13:1-52;
Mk
4:1-34;
Lk
8:4-18;
Zab
78:2;
Isa
6:9,10).
Kanisa siku za mwanzo
Umoja wa waamini na Kristo ndio lengo la Ukristo.
Jumuia ya Wakristo inaitwa
Kanisa
, yaani "mkusanyiko" kama lilivyotajwa na Yesu mwenyewe hasa katika
Injili ya Mathayo
16:18: "Wewe ndiwe
Petro
na juu ya mwamba huu, nitalijenga kanisa langu. Wala milango ya kuzimu haitalishinda".
Yesu aliita wengine 11 pamoja na Petro kuunda kundi la
mitume wake
. Idadi yao ilipangwa kwa kusudi la kudokeza kwamba ndiyo mwanzo mpya wa
taifa la Mungu
, kama vile watoto 12 wa
Yakobo Israeli
walivyokuwa mwanzo wa
taifa
lake la kale.
Yesu aliwapa hao
Thenashara
mamlaka
ile aliyopewa na
Mungu Baba
ili kuokoa watu.
Yesu na wanafunzi wake wa kwanza walikuwa Wayahudi. Yaani walizaliwa katika uzazi wa Abrahamu wakiwa watoto wa Agano lililofanywa kati ya Mungu na taifa lake la Israeli zamani za Musa.
Wakati wa Yesu Waisraeli hao waliitwa "Wayahudi". Walio wengi waliishi nje ya nchi ya Israeli/Palestina, kutokana na
vita
vingi vya zamani vilivyosababisha
wakimbizi
kuhamia nchi zenye
usalama
zaidi. Jumuiya za Wayahudi zilipatikana katika miji yote mikubwa ya
Afrika Kaskazini
(hasa
Misri
na
Libia
),
Ulaya Kusini
na
Asia Magharibi
mpaka
Uajemi
Kwa upande mmoja Wayahudi walitoka katika
ukoo
wa Ibrahimu, hasa waliokaa Israeli/Palestina. Lakini watu wengine wenye asili ya mataifa tofauti waliwahi kujiunga na
imani
ya Wayahudi na kuchukua hatua ya kuongoka na
kutahiriwa
Katika mazingira yao Wayahudi walikuwa watu wa pekee waliomshuhudia Mungu mmoja tu. Walikuwa tofauti na wengine kwani hawakushiriki katika
ibada
ya
miungu
ya
serikali
, tena walitunza
utaratibu
wa
sabato
yaani kutotenda kazi siku ya saba.
Mitume wa Yesu walizunguka awali hasa katika jumuiya za Wayahudi kila mahali walipokwenda. Mwanzoni Kanisa lilionekana kama
dhehebu
la Kiyahudi tu. Baada ya kupokea watu kutoka mataifa bila kuwatahiri hali ilibadilika: Kanisa likawa
taifa la Mungu
kutoka kwa Wayahudi na kwa Mataifa.
Ujio wa
Roho Mtakatifu
Mara baada ya Yesu kwenda zake katika tukio linalotajwa kupaa kwake mbinguni, wafuasi wake wakarudi
Yerusalemu
, yapata mwendo wa
sabato
, na walipoingia huko, wakapanda ghorofani walipokuwa wakikaa
Mtume Petro
na
wenzake
Hata ilipotimia siku ya
Pentekoste
walikuwapo wote mahali pamoja. Ukaja
upepo
toka juu kama upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukatokea na ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa
lugha
nyingine, kama Roho alivyowajalia. (
Mdo
1:12-14, 2:1-4).
Hii ilifuatiwa na Petro na wenzake kuanza kuhubiri
ufufuko
wa
Bwana
Yesu na hatimaye kugusa watu 3,000 waliokubali kubatizwa siku hiyo. (Mdo 2: 37-40).
Ustawi wa jumuia ya kwanza ya wafuasi wa Kristo
Watu walipokuwa wakidumu katika fundisho la mitume,
sala
kumega mkate
na katika
ushirika
, wengi wakaona ishara zao nyingi basi nao wakauza
mali
zao, na vitu walivyokuwanavyo, na kugawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja.
Basi, siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya
hekalu
, wakila pamoja na kushiriki kwa moyo mweupe.
Hivyo ndivyo jumuia ilivyozaliwa na kufahamika kama Kanisa. (Mdo 2:42-47).
Kukutanika na kushiriki ma
fumbo
makuu, kushukuru na kusifu, pamoja na uwepo wa
vipaji
na
karama
za Roho Mtakatifu, hufanya Kanisa liwe hai.
Uenezi wa awali wa Kanisa
Ujumbe
wa Yesu ulienea haraka toka
Yerusalemu
hata
Lida
Yafa
Kaisaria
Samaria
Damasko
n.k. na kuanzisha jumuia nyingi.
Nazo jumuia kwa bidii za waamini wa mwanzo zikafika
Foinike
Kipro
Antiokia
, ambako waliitwa Wakristo kwa mara ya kwanza, kutokana na waamini wa mataifa mengine kuwazidi wale wenye asili ya Kiyahudi (Mdo 11:1-23).
Imani na desturi za mikusanyiko hiyo zenye asili ya Kiyahudi zilitapakaa na hivyo kuanza kusuguana na mapokeo ya jamii mbalimbali zilipopenya. Hii inatokana na ukweli kwamba watu wengi wa siku zile tayari walikuwa na imani zao walizokuwa wakizitunza.
Basi ukaja wakati ambao Wakristo wakaanza kukosoana kuhusu
dhamiri
zao na
huduma
. Ndiyo asili ya
nyaraka
mbalimbali ambazo zinaunda sehemu muhimu wa Agano Jipya.
Uongozi wa Kanisa
Kila
jumuiya
inatumia
mbinu
zake za
uongozi
. Mkuu wa jumuiya ya wanafunzi tangu mwanzo ni Bwana Yesu. Lakini kama kundi ni kubwa kazi ya uongozi ni tofauti. Haiwezekani kufanya kila kitu pamoja watu wakiwa wengi. Ipo lazima ya kugawana
kazi
na
madaraka
Suala
hili limekuwa muhimu sana katika historia ya Ukristo. Njia mbalimbali za uongozi ambazo zilitafutwa na kujaribiwa zinaonyesha tofauti muhimu kati ya madhehebu mbalimbali. Kwa jumla njia hizo zote zinajaribu kuiga mifano ya ushirika wa kwanza inayopatikana katika Biblia. Vyeo na
shughuli
maalumu zilizopo katika Ukristo leo, vina asili na mwanzo katika ugawaji wa madaraka ulivyokuwa wakati wa mitume.
Katika nyaraka za Paulo (ambazo ni maandiko ya kwanza katika Agano Jipya) tunaona hali ya Ukristo mwanzoni kabisa. Paulo anataja mitume, manabii, walimu, wenye vipawa mbalimbali (1Kor 12,28 n.k.), au ma
askofu
na ma
shemasi
, pia
wazee
. Kwa jumla hakuna picha kamili ya
utaratibu
mmoja uliokuwepo kila mahali.
Katika ushirika wa kwanza kule Yerusalemu Mitume, yaani ma
rafiki
wa Yesu wa karibu waliotumwa naye na kupewa kazi ya kueneza Habari Njema, ndio waliokuwa viongozi. Lakini baada ya muda mfupi kazi zilikuwa nyingi, hivyo wakaongeza "
Wasaidizi saba
". Hao saba walishughulikia hasa
huduma
za
upendo
, yaani kuwagawia
wajane
na wazee misaada.
Baada ya Mtume Petro kuhama Yerusalemu,
Yakobo Mdogo
ndiye aliyeongoza ushirika huo.
Mwishoni mwa
karne ya 1
cheo
cha "Askofu" kiliimarika sana, lakini pia vikundi vya Wakristo wenye vyeo maalumu vya
utumishi
vilianza kutokea. Pamoja na Askofu vyeo vya
Kasisi
na
Shemasi
vilikuwa kawaida. Ma
shemasi wa kike
walipatikana pia mwanzoni, lakini walipotea baadaye, kutokana na
utamaduni
uliokazia
kipaumbele
cha
wanaume
Kuanzia mwaka
100
hivi Kanisa likaitwa "
katoliki
" maana yake Kanisa moja kwa ajili ya nchi zote na watu wote, tofauti na vikundi vilivyojitenga nalo. Kila mji ulikuwa na askofu wake aliyeongoza kanisa. Maaskofu wa eneo au mkoa mmoja walikuwa chini ya
Askofu Mkuu
. Maaskofu wa
Roma
Ulaya
hadi Afrika Kaskazini-Magharibi),
Aleksandria
Afrika
) na
Antiokia
Asia
), waliheshimiwa kuliko maaskofu wengine wote wakaitwa "
Papa
" na "
Patriarki
". Cheo cha Patriarki kilipatikana pia kwa Askofu wa
Bizanti
(leo nchini
Uturuki
) baada ya ma
kaisari
wa Roma kuhamia kule, na vilevile kwa Askofu wa Yerusalemu.
Katika karne za baadaye vikundi mbalimbali vilianza kupinga kuwapo kwa vyeo maalumu vya utumishi. Walisisitiza zaidi "
ukuhani
wa Wakristo wote" maana yake kila Mkristo hushiriki utumishi ulio mmoja tu katika Kanisa. Madhehebu mengine ya Kiprotestanti, yakikumbuka sana matatizo ya utaratibu wa kiaskofu wakati wa
karne za kati
, yaliona afadhali kuendelea bila cheo hicho. Wakatoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki pamoja na
Wamoravian
na
Waanglikana
wamehifadhi
ngazi
za kale yaani Uaskofu, Ukasisi na Ushemasi. Nchini
Tanzania
Walutheri
pia
Wabatisti
wa aina ya A.I.C. wanaheshimu cheo cha Uaskofu. Lakini kimataifa sehemu kubwa ya Walutheri, na hasa
Wapresbiteriani
(Reformed) na Wabatisti hawana Askofu, wakisisitiza zaidi
uwezo
na
haki
ya kila Mkristo kushiriki katika shughuli zote za utumishi akichaguliwa.
Imani
ya Ukristo ni juu ya Yesu. Alikuja kwelikweli hapa duniani. Alichagua kuja katika nchi ile ya Israeli miaka 2000 iliyopita. Akawachagua wanafunzi wake ambao tunawaita "mitume". Hakika alikuwa na maana kufanya hivyo. Mitume ndio waliotekeleza maagizo ya Yesu, "Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyoamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dhahari" (
Math
28:19-20). Biblia inatupa habari za aina hii: wale Mitume ni mifano ya Ukristo wetu katika nguvu au
karama
zao, lakini pia katika
udhaifu
wao.
Petro
Petro ni jina lenye maana ya "
mwamba
". Alikutana na Yesu akiwa
mvuvi
, akaendelea kuwa rafiki yake wa karibu sana. Yesu alipokamatwa, Petro alitaka kutumia
upanga
wake ili amtetee. Lakini alipoulizwa baadaye kama yeye ni rafiki wa Yesu aliogopa akasema hamjui.
Katika ushirika wa Yerusalemu alikuwa kiongozi muhimu. Alikuwa Mtume wa kwanza kumpokea katika Kanisa watu wasio Wayahudi bila kudai
watahiriwe
kwanza. Baadaye akawa katika mji mkubwa wa
Antiokia
. Katika taarifa ya Luka tunamwona tena Yerusalemu alipokutana na Paulo na kushauriana juu ya kupokea Wapagani katika Ukristo.
Agano Jipya ina nyaraka mbili zilizoandikwa kwa jina lake. Kumbukumbu ya kale inasema alifika mpaka
Roma
. Hapo aliuawa pamoja na Paulo katika mateso ya kwanza ya Wakristo chini ya
serikali
Petro ni mfano mzuri wa nguvu na udhaifu katika maisha ya Kikristo. Alikuwa na
moyo mkuu
kumtetea Yesu kwa upanga asikamatwe - lakini mpaka siku ile hakuelewa kwamba njia ya Yesu si njia ya
silaha
. Alitaka kuwa karibu na Yesu - lakini kwa
hofu
akamkana. Alimwingiza katika Kanisa
jemadari
Mpagani - lakini baadaye akawaogopa waliosema kwamba Mpagani asiingie katika ushirika mpaka awe ametahiriwa na kuwa Myahudi kwanza. Mwishoni mwa maisha yake Petro akawa
shahidi
wa
damu
kwa Bwana wake kule Roma akafa msalabani kama Yesu.
Kanisa la Roma
linamkumbuka kama askofu wake wa kwanza. Kila
Papa
wa Kanisa Katoliki huitwa "mwandamizi wa Petro" kwani anashika cheo cha Askofu wa Roma kinachoaminika kuwa cha kwanza kati ya maaskofu wote duniani.
Paulo
Nyumba ya
Mt. Anania
Damasko
Syria
, ni kati ya zile za kwanza kutumika kwa ibada katika karne ya 1.
Paulo hakuwa mfuasi wa Yesu alipokuwa duniani. Alikuwa Myahudi
Farisayo
mzaliwa wa
Tarso
(mji wa
Kilikia
, leo nchini
Uturuki
). Alikwenda Palestina kwa masomo ya kidini. Tunasikia habari zake alivyohusika na
kifodini
cha
Stefano
(Mdo 6).
Baadaye akatumwa na
Baraza Kuu la Kiyahudi
kuwatafuta Wayahudi waliojiunga na Ukristo na kuwakamata kama wakosaji. Aliposafiri hadi
Dameski
(mji mkuu wa
Siria
) kwa ajili hiyo, Yesu alimtokea katika
ono
akaongoka kuwa Mkristo. Hivyo mtesaji wa Wakristo akawa
mhubiri
mkuu wa Injili.
Hakuna mwingine kati ya mitume wote aliyesafiri, kuhubiri na kuanzisha shirika kama Paulo. Katika
safari
kubwa tatu alizunguka
Asia Magharibi
na
Ulaya Kusini
. Akaendelea kufundisha shirika alipoondoka kwa njia ya
barua
(au
nyaraka
).
Nyaraka zake
mbalimbali zimehifadhiwa katika Agano Jipya. Katika nyaraka hizo Paulo anaonekana kuwa mtaalamu wa
Sheria ya Kiyahudi
ilivyo katika
Agano la Kale
. Akatetea kupokea Wapagani katika Kanisa akafundisha jinsi gani
uhuru
katika Kristo unavyopita masharti ya sheria ya kale.
Mwishoni akakamatwa kule Yerusalemu akashtakiwa ya kuwa amehatarisha
amani
. Kama mzaliwa wa Tarso alikuwa na
uraia
wa Roma akadai
haki
yake ya kukata
rufaa
kule, mbele ya
Kaisari
. Akapelekwa Roma (Mdo 28). Hatuna hakika juu ya
kesi
yake. Labda alipata nafasi ya kusafiri tena na kuhubiri Injili mpaka
Hispania
. Lakini kumbukumbu ya kale inatuambia kwamba aliuawa baada ya Petro kwa kukatwa kichwa katika mateso ya kwanza ya Wakristo (
64
68
BK).
Paulo ni mfano mzuri jinsi gani mtu aliyepinga Injili vikali aliongozwa kuihubiri. Nyaraka zake zinatuonyesha jinsi gani Mkristo anaweza kutumia
akili
yake pamoja na imani. Katika maandishi yake tunapata mtu aliyebebwa na imani katika matatizo na mateso makubwa. Anatufundisha kutoangalia Ukristo kama sheria au
amri
tu (Fanya! Acha!) bali kama jibu la
upendo
la mtu aliyeelewa upendo wa Mungu kwanza.
Thoma
Mtume anayekumbukwa sana kule
India
ni
Thoma
(au: Tomaso) aliyefika mpaka Bara Hindi.
Kaburi
lake huonyeshwa katika mji wa
Madras
. Mpaka leo wako "Wakristo wa Thoma" kusini-magharibi mwa Bara Hindi. Kwa muda mrefu walikosa mawasiliano na Wakristo wengine waliokuwa mbali, lakini siku hizi wanashiriki katika
umoja wa Kanisa
duniani.
Muhtasari wa historia ya Kanisa
Makala kuu:
Historia ya Kanisa
Samaki
ilipata kuwa ishara ya Ukristo, kutokana na jina lake la Kigiriki lililoandikwa hivi huko
Efeso
Uturuki
Ukristo ulianza Mashariki ya Kati kama madhehebu ya Uyahudi ukaenea haraka kwa watu wa mataifa mengine mengi ya Asia, Afrika na Ulaya hivi kwamba waamini wenye asili ya Kiyahudi walizidi kuwa asilimia ndogo hasa kufikia mwisho wa
karne ya 1
Kwa juhudi za Mitume waliowahi kuchaguliwa na Yesu na za wengineo, hasa Mtume Paulo.
Ukristo ulienea hasa ndani ya mipaka ya
Dola la Roma
na kupokea yaliyo mema kutoka umataduni hasa wa Wagiriki (mashariki) na Walatini (magharibi), bila kukwamishwa na
dhuluma
za
serikali
zilizodumu kwa
kwikwi
miaka karibu 250 (
64
313
).
Hata nje ya dola hilo, Ukristo ulikabiliana na dhuluma, kama vile
Mesopotamia
na
Uajemi
, ambapo ulidumisha zaidi sura asili ya
Kisemiti
Wakati wa maisha ya Mitume, dhuluma zilizotabiriwa na Yesu zilianza kutoka kwa Wayahudi wasiomuamini na kutoka kwa watu wengine. Wa kwanza kuuawa alikuwa Stefano, na kati ya Mitume Yakobo Mkubwa. Kabla ya kufa, wengi kwa kuuawa, mitume waliweka waandamizi wao, ambao kati yao maaskofu mwanzoni mwa karne ya 2 walikuwa wameshika uongozi wa makanisa wakisaidiwa na mapadri na mashemasi.
Wakati huohuo vitabu vingi vya Kikristo vilivyotungwa katika nusu ya pili ya karne ya 1 vilizidi kuenea na kukusanywa hadi vikaunda Agano Jipya.
Baada ya hapo vitabu viliendelea kuandikwa kwa kutetea, kutangaza na kufafanua imani sahihi: ndiyo mwanzo wa teolojia kama fani maalumu. Tofauti za ufafanuzi huo, kama zile kati ya shule ya Aleksandria na shule ya Antiokia, ndizo chanzo cha mabishano yaliyochangia mafarakano makubwa yaliyotokea hasa katika
karne ya 5
, ingawa kuanzia mwaka
325
mitaguso mikuu
ilikusanya maaskofu wengi kutoka sehemu mbalimbali ili kumaliza migogoro. Tofauti za
lugha
na utamaduni, pamoja na
utaifa
, zilichangia sana ma
farakano
Monasteri
ya
Khor Virap
(karne ya 7) ikiwa na
Mlima Ararat
nyuma yake, Armenia.
Maendeleo mengine muhimu yalipatikana katika
maisha ya Kiroho
kwa uanzishaji wa
umonaki
wa Kikristo, kwanza katika majangwa ya
Misri
, halafu sehemu nyingine zote.
Juhudi
za watu hao zilichochea waumini wenzao pia kuwa waaminifu katika
ulimwengu
uliozidi kuwashawishi badala ya kuwatesa.
Ni kwamba kufikia mwisho wa
karne ya 4
Ukristo ulikuwa
dini rasmi
ya
Dola la Roma
ambalo kabla ya hapo kwa miaka karibu 250 (
64
313
) lilikuwa limeukataza kikatili. Kabla yake
Armenia
ilikuwa nchi ya kwanza kupokea Ukristo kama
dini ya taifa
301
).
Ushindi
huo ulifanya wengi watamani vyeo ndani ya Kanisa, kwa kuwa viliendana sasa na heshima na
mali
: hivyo ubora ulipungua.
Dola la Roma Magharibi lilipozidi kudhoofiwa na uvamizi wa
Wagermanik
na makabila mengine yasiyostaarabika, askofu wa Roma kama mchungaji mkuu alilazimika kuwajibika ili kuokoa jahazi. Ndivyo walivyofanya hasa
Papa Leo I
na
Papa Gregori I
. Kwa juhudi za wamonaki
Wabenedikto
na wengineo, ustaarabu wa kale uliokolewa katika vitabu vyake na
uinjilishaji
uliendelea katika Ulaya ya Kati.
Picha kadhaa zikionyesha Wakristo maarufu na athari ya Ukristo katika utamaduni.
Kumbe, uenezi wa
Uislamu
kuanzia
karne ya 7
ulidhoofisha na pengine kukomesha kabisa Ukristo katika nchi nyingi, ukirudisha nyuma ustawi wa Kanisa lote. Hata hivyo,
mwanzoni mwa karne ya 8, Uislamu ulizuiwa na
Wafaranki
kuenea zaidi Ulaya bara. Kabila hilo kubwa la Kigermanik liliwahi kujiunga na Kanisa Katoliki likawa msaada mkubwa kwa Mapapa. Isipokuwa kwa kuwaachia watawale
Italia ya Kati
, walisababisha Papa aanze kuwa kama mfalme wa dunia hii, jambo lililoathiri sana majukumu yake ya kiroho hadi mwaka
1870
Katika
Karne za Kati
Ulaya yote ilikwisha kuwa ya Kikristo. Kutoka huko ulienea, pamoja na
ustaarabu wa magharibi
ulioathiriwa sana na Ukristo, katika
Amerika
yote na sehemu nyingine za dunia.
Mafarakano makuu kati ya Wakristo
Matawi ya Ukristo yalivyotokea katika
historia ya Kanisa
. Upande wa juu ndio Kanisa la Magharibi, upande wa chini Makanisa ya Mashariki. Unene wa mistari haulingani na ukubwa wa madhehebu husika.
Ibada ya pamoja katika
monasteri
ya
kiekumeni
Taizé
Ufaransa
Katika historia ndefu ya Ukristo, yalitokea mafarakano mengi, waamini wa Yesu wakizidi kutofautiana. Makundi makubwa zaidi ni:
Kanisa Katoliki
, Makanisa ya
Waorthodoksi
na ya
Waorthodoksi wa Mashariki
na
madhehebu
ya
Uprotestanti
. Hasa tangu mwaka
1910
madhehebu mengi yanashiriki juhudi za
ekumeni
kwa ajili ya kurudisha umoja wa awali.
Wakatoliki
Zaidi ya nusu ya Wakristo wote wanashikamana katika
imani
na
sakramenti
chini ya ma
askofu
wenye
ushirika kamili
na yule wa
Roma
, ambaye kwa kawaida anaitwa
Papa
Kati yao
umoja
unazingatiwa sana kama sifa ya kwanza ya Kanisa inayotambulisha wanafunzi wa Yesu.
Neno "Katoliki" tunaendelea kulitumia zaidi kwa maana ya madhehebu maalumu yenye wafuasi wengi duniani. Kiteolojia linamaanisha "Kanisa lililopo popote, lililo moja tu kila mahali na kila wakati". Kwa maana hiyo kila Mkristo yumo katika Ukatoliki, kwani mbele ya Kristo Kanisa ni moja tu, kila mahali duniani.
Waanglikana
Walutheri
Wamoravia
na wengineo huamini kabisa kwamba wenyewe ni sehemu ya Kanisa lile moja la Bwana Yesu lililopo mahali popote.
Upande mwingine, hata Kanisa “Katoliki" linaloongozwa na Askofu (Papa) wa Roma ni la "Kiinjili" kwani linakubali na kutangaza Injili (= “habari njema”) ya Yesu Kristo.
Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki
Kanisa kuu
la Kristo
Mwokozi
huko
Moscow
ni refu kuliko yote ya
Waorthodoksi
duniani.
Wakristo wengi walioishi upande wa mashariki wa
Dola la Kirumi
na
ng'ambo
ya mipaka yake ya mashariki walitengana na Wakatoliki hasa katika
karne V
Waorthodoksi wa Mashariki
) na
karne XI
(Waorthodoksi).
Hata hivyo msimamo wao wa imani si tofauti sana, kwa kuwa wanachanga
mapokeo
ya awali ya
Kanisa la Mitume
na la
Mababu
Waprotestanti
Utitiri
wa madhehebu ya
Waprotestanti
ndio wenye tofauti kubwa zaidi kati yao wenyewe na kati yao na Wakristo waliotajwa kwanza.
Hiyo ilitokana na msimamo wa msingi wa
urekebisho wa Kiprotestanti
wa kutaka kila mmoja aweze kutafsiri
Biblia
alivyoielewa, bila kutegemea mapokeo wala
mamlaka
rasmi ya Kanisa, ila msaada wa Roho Mtakatifu.
Umoja
halisi wa Kanisa unaweza kupatikana tu katika ukweli wa Injili ya Yesu Kristo. Ni habari mbaya kwamba katika
karne ya 16
kuupigania
ukweli
huo kulivunja umoja wa
Ukristo wa magharibi
. Haiwezekani kushangilia mafarakano ya wafuasi wa Yesu.
Yale ya karne hiyo yalitokana na kuelewa tofauti kweli za imani ya Kikristo na yalikuwa na ukali kwa sababu pande zote zilisadiki kwamba kushikilia kwa usahihi
ufunuo
wa Mungu ni suala la
wokovu
wa milele. Kwa mfano,
Martin Luther
aliandika,«Sikubali mafundisho yangu yahukumiwe na yeyote, hata kama ni malaika. Asiyekubali mafundisho yangu hawezi kufikia wokovu».
10
Pamoja na hayo, mambo mengi yalichangia farakano, si
teolojia
tu, bali
siasa
uchumi
jamii
na
utamaduni
. Wakati huo mara nyingi
hoja
za imani na malengo ya kisiasa vilichanganyikana: wanasiasa wengi walitumia hoja hizo ili kufikia malengo ya kiutawala, na vilevile
wanateolojia
walitumia siasa kutetea mafundisho yao ili kuvuta watu. Ndiyo sababu Luther alichorwa kama
shujaa
wa
taifa
la
Ujerumani
Mara nyingi pande zote zilipotosha maana ya wapinzani na kuwachora vibaya wakivunja amri ya nane inayokataza
uongo
dhidi ya jirani. Hata waliojitahidi kusema ukweli tu juu ya wengine kwa kawaida hawakujitahidi vya kutosha kuelewa msimamo wao na kuona kwamba pengine si mbaya zaidi. Kila mmoja alitaka
ushindi
akachangia
ugomvi
uliorithishwa kwa vizazi vilivyofuata.
Hivyo, kilichosababisha zaidi farakano si masuala ya imani yaliyojadiliwa na Waprotestanti, bali
lawama
zao dhidi ya hali mbaya ya Kanisa la wakati huo iliyokuwa inakera wengi na kuwaelekeza kuunga mkono
urekebisho
Hapo kale neno hilo (kwa Kilatini reformatio) lilihusu badiliko la hali mbaya iliyopo ili kurudia hali nzuri zaidi ya awali. Katika
Karne za Kati
lilitumika mara nyingi kwa marekebisho ya
umonaki
. Katika
karne ya 15
haja ya urekebisho ilionekana wazi si tu kwa mashirika ya kitawa bali kwa Kanisa lote. Hasa
Mtaguso wa Konstanz
1414
1418
) ulidai kabisa ufanyike «katika
kichwa
na katika
viungo
». Lakini kwa jumla mitaguso yote ya Karne za Kati na mikutano mingi ya
Bunge
la
Dola la Ujerumani
ililenga urekebisho wa Kanisa.
Kwa kweli Karne za Kati zilikuwa na mchanganyiko wa mambo yaliyopingana:
ibada
za nje tu na za dhati kabisa;
teolojia
iliyoelekeza kutenda kwa msingi wa nipe nikupe na hakika ya kwamba
binadamu
anategemea kabisa
neema
ya Mungu; kutojali
wajibu
hata upande wa viongozi wa Kanisa na marekebisho safi ya mashirika ya kitawa.
Karne ya 15
ilikuwa kipindi cha
umotomoto
wa pekee katika Kanisa, ambapo
walei
wengi zaidi na zaidi walipata elimu nzuri, hivyo walitamani
hotuba
bora na mafundisho ya kuwasaidia kuishi Kikristo zaidi. Luther aliitikia haja hizo zilizomgusa sana kama mtu wa wakati wake.
Luther alitumia kwa nadra neno urekebisho, lakini likaja kuwa jina la kawaida la matukio yale mengi ya miaka
1517
1555
, yaani kuanzia uenezi wa
hoja 95
za Martin Luther hadi
amani ya Augsburg
. Kati yake chanzo, yaani mabishano ya Kikanisa yaliyosababishwa na teolojia ya Luther, yalichanganyikana mapema na siasa, uchumi na utamaduni, kutokana na hali halisi ya wakati huo, mbali kuliko mwenyewe alivyofikiri.
Viongozi mbalimbali wakaiga mfano wa Luther, ila juhudi zao zikatofautiana: ndio mwanzo wa madhehebu mengine yanayoitwa ya "Kiinjili". Jina hilo linataka kusisitiza kwamba yanasimama kwenye msingi wa Injili tu, kinyume cha Kanisa Katoliki lililoona mapokeo yake kuwa na umuhimu pamoja na Biblia.
Kumbe wafuasi wa Luther na wengineo waliitwa na Wakatoliki "Waprotestanti", maana yake "wapinzani" (to protest = kupinga): neno hilo lilianza kutumika tangu wafuasi wa Luther walipopinga azimio la bunge lililotaka Wajerumani wote warudi chini ya Papa wa Roma.
Tangu mwaka
1907
tapo la
Wapentekoste
limeenea duniani kote (linakadiriwa kuwa na waumini milioni karibu 300) na kuathiri hata madhehebu yote ya zamani (ambapo mara nyingi waumini wa aina hiyo wanaitwa "
Wakarismatiki
").
Kanisa leo
Nchi ambapo Wakristo ni 50% au zaidi zimechorwa rangi ya zambarau, na zile ambapo ni kati ya 10 na 50% zina rangi ya waridi
Nchi ambapo Ukristo ni
dini rasmi
Ukristo wa Kiorthodoksi
Ukristo wa Kiprotestanti (pamoja na Anglikana)
Ukristo wa Kikatoliki
Uwepo wa Wakristo duniani: Rangi nzito inaonyesha asilimia kubwa zaidi ya Wakristo
11
Kwa miaka 100 ya mwisho asilimia za Wakristo kati ya watu wote zimebaki 33, yaani mmoja kwa watatu, lakini
uwiano
kati ya
mabara
umebadilika sana, kwa maana katika Afrika, Asia na
nchi nyingine zinazoendelea
Wakristo wameongezeka, kumbe Ulaya na
Amerika Kaskazini
wamepungua
12
Pew Research Center
inakadiria kwamba mwaka
2050
, watazidi
bilioni
tatu
13
. Wakati huo Wakatoliki na Waprotestanti huenda wakalingana kwa idadi
14
15
Kuhusu maeneo ambako Wakristo wanapungua, ni kwamba, kutokana na
historia ya Kanisa
kuwa na mchanganyiko wa mazuri na mabaya, wengine wanahisi kuwa halina maana tena. Pia kuna makundi kama
Wakomunisti
na
Wamasoni
ambayo yanakusudia kabisa kufuta Ukristo kwa kutangaza kasoro za waumini na viongozi wao, pamoja na kuhimiza watu kwenda kinyume cha
maadili
Hali hii inajionyesha hasa pale ambapo waamini wengi, hasa Ulaya, wameacha kwenda kanisani isipokuwa siku ya
Krismasi
na
Pasaka
au kwenye
harusi
na misiba.
Pia kutokana na mgawanyiko wa madhehebu, kumekuwa na mkanganyiko kuhusu kazi ambazo zinalipasa Kanisa la leo.
Sala na ibada
Padri akiadhimisha
Misa
katika
Basilika
la
Bikira Maria
Bangalore
India
Mafundisho ya Yesu kuhusu
sala
hayatii maanani taratibu maalumu. Badala yake yeye alisisitiza msimamo wa ndani wa kumuendea Mungu kwa imani na
unyofu
kama vitoto wanavyohusiana na baba zao. Ndivyo mwenyewe alivyosali katika Roho Mtakatifu aliyewaahidia wafuasi atawaongoza badala yake.
Kwa msingi huo, katika historia ya Kanisa namna nyingi za kusali zimetokea kwa
maisha ya Kiroho
ya Mkristo binafsi na kwa jumuia nzima pamoja. Kwa kawaida, taratibu za kuendesha ibada zinaitwa
liturujia
(kutoka maneno ya Kigiriki yenye maana ya “kazi ya hadhara”).
Wakatoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki,
Waanglikana
Wamethodisti
Walutheri
na wengineo wanafuatilia desturi kama walivyozipokea. Mtiririko wa
ibada
zao huandikwa na hujulikana kama
Liturujia
Bendi
ya Kiprotestanti ikiongoza ibada inayofanana na tamasha.
Madhehebu mengine, hasa yale ya
Kipentekoste
, huwa na ibada ambazo hazijaandikwa kitabuni: kiongozi wa ibada wa siku hiyo huja na madondoo yake na mtiririko wa ibada huenda kama "Roho" atakavyoongoza siku hiyo. Kwa sababu hiyo husema kwamba hawafuati desturi au mapokeo.
Ukiangalia zaidi utaona kuwa ibada zao pia huwa na mtindo na mtiririko fulani, kama vile kuimba mapambio ya harakaharaka wakiwa wanapiga makofi, kucheza na kurukaruka. Mapambio hayo hufuatiliwa na mengine ya taratibu wakiinua mikono
kuabudu
. Inawezekana kusema hao nao wana utaratibu au liturujia yao ingawa haijaandikwa kwenye vitabu.
Wakristo wanahesabu ufufuko wa Yesu kuwa msingi mkuu wa imani yao (1Kor 15:14): ndiyo sababu karibu wote wanaabudu hasa
Jumapili
, ambayo ndiyo siku ya tukio hilo kuu la
historia
yote. Ila
asilimia
1 inashika
Sabato
, iliyo siku ya wiki ambapo Wayahudi hupumzika na kuabudu.
Haki na amani
Mama Teresa
wa
Kolkata
Upande mwingine wanakanisa wanajaribu kuonyesha jitihada zao katika jamii, ikiwa ni pamoja na kuleta
amani
na
maendeleo
na kutoa misaada ya kijamii. Kuna uwezekano kwa madhehebu kadhaa kubadilisha mkazo wao kuutoa kwenye imani tu na kuuweka kwenye huduma za jamii au elimu: hii inafanya yaonekane kama moja ya mashirika ya hisani.
Katika nchi nyingi Kanisa limekuwa nguvu ya kutetea
haki za binadamu
. Tumesikia habari za
Desmond Tutu
kule
Afrika Kusini
au za
Janani Luwum
katika
Uganda
, jinsi walivyojaribu kutetea haki za wananchi dhidi ya utawala mbaya. Ikiwa Wakristo wanajisikia wito wa kusimama na kusema mbele ya wakubwa hukumbuka manabii wa
Agano la Kale
hadi
Yohane Mbatizaji
. Wanakumbuka pia Wakristo wengi katika historia walioweza kusimama mbele ya wafalme na kutetea haki za watu. Labda tunamkumbuka Askofu
Ambrosi
wa
Milano
(aliyemvuta kijana
Agostino
kuwa Mkristo) alivyomtenga
Kaisari
na Kanisa kwa sababu ya
uuaji
wa wananchi wengi wasio na kosa uliofanywa na wanajeshi wa serikali. Msingi wake ni katika mafundisho juu ya kazi ya uumbaji. Mbele ya Mungu tuko sawa: kuna msingi gani kuona wengine ni sawa zaidi?
Lakini si Wakristo wote wanakubali na kufurahia msimamo wa aina hiyo. Wengine huona imani ya Kikristo haihusiki na taratibu za dunia hii au huona ni wajibu wa Mkristo kutii serikali yoyote wakikumbuka maneno ya Mtume Paulo katika
Rum
13. Pamoja na hayo katika Ukristo yapo mapokeo ya kutoshindana na wenye
mamlaka
bali kuwavumilia katika yote. Labda huona hofu ya kuwa dini inaingizwa mno katika
siasa
Binadamu wa
karne ya 21
wanahitaji jibu litakalosaidia kuwakwamua kutoka matatizo yao. Wenye dini mbalimbali, hususan Wakristo, wanadai kujua ufumbuzi wa matatizo makuu ya binadamu, ingawa wachache tu wameweza kuonyesha dhahiri matatizo yaliyotatuliwa kabisa kwa dini. Wakati mwingine wanadini wenyewe wamekuwa chanzo cha matatizo badala ya kuyatatua.
Jibu linaweza kupatikana katika maneno ya Yesu mwenyewe, aliposema kwamba wafuasi wake ni chumvi ya dunia, ambayo ilete ladha katika maisha ya watu, lakini kama chumvi hiyo inapoteza ladha yake, haifai kitu, isipokuwa kutupwa na kukanyagwa kwa dharau. Hivyo changamoto ya Wakristo ni kufuata vema mafundisho ya imani yao ili kukidhi hitaji la nyakati hizi la kuishi kwa amani, furaha na upendo duniani kote .
Uhusiano na dini nyingine
Ukristo na dini nyingine zinahusiana kwa kiasi tofauti, kadiri ya
mazingira
asili,
historia
, mafundisho kuhusu
imani
na
maadili
desturi
ibada
n.k.
Ukristo na Uyahudi
Ni wazi kuwa
Ukristo
unahusiana zaidi na
dini
ya
Uyahudi
, kwa sababu unatokana nayo na kutumia vitabu vyake vitakatifu (
Tanakh
na pengine
Deuterokanoni
pia). Haiwezekani kumuelewa
Yesu
kwa kumweka nje ya mazingira ya Kiyahudi.
Dini hizo mbili zilitengana moja kwa moja miaka 50 hivi baada ya Yesu kuaga dunia. Ni kwamba Wayahudi wa
shule ya Jabneh
(mwaka
80
hivi
B.K.
) waliamua kuwatenga kama
wazushi
wananchi wenzao waliomuamini
Yesu Kristo
, hasa baada ya kuona hawakusaidia
vita vya ukombozi
dhidi ya
wakoloni
Warumi
vilivyosababisha maangamizi ya
Hekalu la pili
na
mji
wa
Yerusalemu
mwaka
70
B.K.
Tangu hapo Wakristo hawakushiriki tena ibada pamoja na Wayahudi, wakazidi kuzingatia
sakramenti
ya
Kumega Mkate
katika
Siku ya Bwana
Jumapili
, siku inaposadikika Yesu alifufuka) badala ya
Sabato
Jumamosi
, siku ya
pumziko
ya Wayahudi). Kabla ya hapo
Wakristo wa Kiyahudi
walikuwa wanashika siku zote mbili.
Ukristo na Ubuddha
Hakuna uhusiano wa kihistoria kati ya Yesu na
Ubuddha
. Hata hivyo mambo kadhaa yanafanana.
Yesu alifundisha kuhusu
nidhamu
mbili zinazompelekea mtu kuwa
mwadilifu
na hatimaye kuurithi
utukufu
wa kiroho ambao
karama
yake ni
uzima wa milele
: hizo ni kumpenda
Mungu
kwa
moyo
wako wote na kwa
akili
yako yote na kwa
nguvu
zako zote, na
jirani
yako kama unavyojipenda mwenyewe.
Buddha
alifundisha hali ya kutodhuru
viumbe hai
wowote, tena kuwa na
moyo mkuu
wa
mapenzi
kwa vitu vyote. Hii ni miongozo inayolenga mtu atambue
tabu
anazodumisha yeye mwenyewe, kwa matendo yake na
upeo
ulio na mipaka, katika
maisha
yake ya kila siku.
Baada ya hili, mafundisho ya
Kristo
yanatofautiana katika kuchukulia hali hii. Kwa mujibu wa Kristo,
dhambi
, matendo yenye kukosea kanuni za kiroho na hata za ki
maumbile
, hufutwa na
toba
; wakati katika mafundisho ya Buddha, makosa yote yanatokana na kutokuwa makini. Hivyo, kwa mujibu wa Buddha, njia pekee ya kumkomboa mtu na shida zake ni kufuata
mwongozo
wa
Nguzo Nane
ambazo humweka katika hali ya kuweza kuamka kiroho wakati
utulivu
wa kimwili na wa kiakili unapofikiwa. Haya ndiyo yanayofanya Ubuddha kuwa ni njia inayojali sana nidhamu ya mtu kimatendo, wakati Ukristo hufuata sana moyo wenye kukiri makosa, na kutafuta uadilifu wa kweli wa kiroho. Huu ni
uzuri
wa pekee kutoka kwenye mafundisho ya Yesu:
Tubuni
kwa kuwa saa ya ukombozi ni sasa...
Jingine lenye tofauti ni kuwa Kristo hufundisha kuhusu
Upendo
kwamba ni Mungu, kwa kuwa Upendo una maana kuliko
elimu
yote ya
binadamu
, nao ndio unaounganisha na kutunza vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Hilo hutambulika kupitia Kristo ambaye hujidhihirisha kwa yule mwenye kumpokea
Roho wa Mungu
. Upande wa Buddha, hukanusha
nafsi
na pia Mungu, akisema: Ni Buddha mwenye
ufahamu
wa milele, tena hana nafsi isipokuwa
Utupu
; na ni wenye
furaha
isiyo kifani izidiyo yote yenye kufanyika
ulimwenguni
, yaani
Nirvana
; kila mtu ni Buddha aliyesahau
asili
yake ya ndani kabisa.
Ukristo na Uislamu
Ukristo na
Uislamu
vinafanana zaidi kwa sababu
Muhammad
alifahamu
Wayahudi
na Wakristo wengi katika nchi yake na katika
safari
zake. Dini hizo tatu zinajulikana kwa kushika imani katika Mungu Pekee,
muumba
wa vitu vyote, na kwa kumchukua
Abrahamu
kama kielelezo cha imani na
rafiki
wa Mungu.
Mafundisho ya msingi ya Uislamu ni
unyenyekevu
kwa
Mola mmoja
aitwaye
Allah
, mwingi wa
rehema
na mwingi wa
fadhila
nguzo
ya Uislamu ni kumuabudu. Katika Uislamu, unyenyekevu wa mtu katika kumcha Mola kwa ibada na
swala
humpa kukirimika na kuhifadhika kwa Mola wake mwenye fadhila, ambaye atamtunuku
haki
yake. Naye mnyenyekevu kwa Mola ataishi kuona utukufu mwingi wa Mola wenye kutajwa katika
Kurani
kwa
majina 99
ya Allah. Kati ya
sifa
na utukufu huo ulio na majina mengi, baadhi yake ni
Al Rahman
(kwa
Kiarabu
, "Mwenye rehema"),
Al Nur
("Mwenye
nuru
") n.k. Hayo hufanana na neno la Nuru ya Bwana, rehema na
ukombozi
kuwa utukufu wa
Mbingu
katika mwongozo wa Kikristo.
Pia Uislamu unafundisha
udugu
miongoni mwa Waislamu yaani
mzizi
wa neno linalotumika sana katika Kurani:
Waly
Wala, Wilayat, Mawla, Awla
) katika kueleza jinsi Mwislamu apasavyo kuishi karibu na mwenzake. Nalo husisitiza upendo na kulindana kwa
heri
na pia kuepushana na
shari
. Hilo linafanana na upendo ambao katika Ukristo ndio
adili
kuu kuliko yote:
Nijaposema kwa
lugha
za wanadamu na za
malaika
, kama sina upendo... mimi si kitu kabisa. (
1 Wakorintho
13:1-11).
Lakini katika Ukristo upendo hauna mipaka wala ma
sharti
. Unatakiwa kuenea kwa ma
adui
pia na kusamehe kila mara kufuatana na mfano wa
Baba
wa Mbinguni.
Mwislamu kadiri ya wingi wa unyenyekevu na
usafi wa moyo
wake huakisi sifa za Mola wake. Uislamu hufundisha kuhusu
vita vya ndani
ambavyo muumini hupigana na nafsi yake yenye matamanio ya chini, ambayo huzaa
chuki
dhuluma
wivu
na maovu mengine ili kuishinda kwa utukufu wa Mola na kudumisha dini (mwongozo) yake katika
ngazi
zote za maisha.
Kabla yake Yesu alihimiza wote wafuate mfano wake wa
upole
na unyenyekevu wa moyo, akitoa kielelezo katika
Heri Nane
za
hotuba ya mlimani
. Tofauti ya msingi ni kuwa kwa mujibu wa Kristo, ni kwa
neema
ya imani katika
Neno la Uzima
kwamba mtu hukombolewa kutoka matamanio yake ya kibinadamu, mbali ya kwamba anapaswa kujitahidi asije akapotewa na neema hiyo na kurudia
utumwa
wa dhambi.
Ni imani ya Wakristo na ya Waislamu kwamba
Yesu atarudi duniani
kwa utukufu, ingawa jambo hilo wanalitafsiri kwa namna tofauti.
Uhusiano wa Wakristo na Waislamu una umuhimu wa pekee kwa ajili ya amani na maendeleo ya nchi. Katika sehemu mbalimbali Wakristo na Waislamu waliwahi kushirikiana vema katika mambo mengi ya kijamii lakini uhusiano huo umeanza kuwa mgumu.
Sababu moja ni mzigo wa historia tunaoubeba mara nyingi bila kujua. Mzigo huo ni urithi wa mahusiano magumu kati ya Waislamu na Wakristo kule Ulaya na Asia. Itakuwa muhimu sana kwa vijana wa leo kukataa mzigo wa historia na kuvumiliana.
Kwa mfano, Waislamu wanaweza kutumia neno "
jihadi
" wakiongea juu ya jitihada za kuimarisha jumuiya yao au kueneza imani yao, lakini Wakristo walio wengi wanasikia neno hilo vibaya kwa sababu "vita vitakatifu" vya Waislamu vilivyoitwa "jihadi" vilileta mateso mengi kwa Wakristo katika nchi mbalimbali. Kumbe neno halimaanishi
vita
hasa ila liliwahi kutumika hivyo tangu muda mrefu.
Vilevile Wakristo wengi hawaoni tatizo kutumia neno "Crusade" kwa ajili ya mikutano ya kiroho. Lakini Waislamu wanaweza kuchukua neno hili vibaya pia kwani kiasili "Crusade" (maana yake "
Vita vya Msalaba
") linamaanisha hasa kipindi cha miaka 800 hivi iliyopita. Wakati ule Wakristo wa
Ulaya Magharibi
walijaribu kufuta utawala wa Kiislamu katika nchi za
Mashariki ya Kati
kwa vita vilivyoendelea kwa
kwikwi
muda wa miaka 200.
Ukristo na Uislamu viko karibu katika mambo mengi lakini hutumia mafundisho yanayogongana katika sehemu nyingine, hivyo mpaka leo hii kwa Waislamu ni vigumu sana kupokea Injili. Wakati wa vita vya msalaba
Fransisko wa Asizi
aliona hakuna njia ya kuwavuta Waislamu kwa mabavu. Mashindano pekee yanayoruhusiwa kwa Mkristo ni yale ya upendo ya kumfuata Yesu.
Kwa jumla mawazo ya Mt. Fransisko yamethibitishwa na historia. Kwa hiyo si vibaya kujiandaa kushirikiana na Waislamu Kikristo kwa kufahamu kidogo imani yao na kutambua sifa nzuri zilizopo katika maisha na mafundisho yao pia.
Wakristo kwa jumla wasijivunie sifa zao kuwa bora kuliko za Waislamu. Anayesoma "Historia ya Kanisa" ataona mifano mingi ya jinsi Wakristo walivyosahau mafundisho ya Yesu na kutendeana kwa unyama. Kwa hiyo mtu asijivune kwamba Ukristo ni dini ya upendo au imani yenye maendeleo kama mwenyewe si mfano wa upendo huo na maendeleo hayo.
Kwa Wakristo wengi ni
fumbo
kwa nini Mungu alikubali kutokea kwa dini hiyo mpya. Lakini mwanzoni mwa Uislamu Mfalme Mkristo wa Ethiopia alipokea na kuhifadhi wakimbizi Waislamu kutoka
Maka
. Mapokeo ya Kiislamu yanasema mfalme huyu aliyekuwa na jina "Negasi" aligeukia Uislamu baadaye. Lakini "Negasi" si jina la mtu fulani, ni cheo cha wafalme wote wa Ethiopia hadi mwaka
1974
(kwa kawaida huandikwa "Negus"). Halafu hakuna kumbukumbu ya kwamba mfalme yeyote wa karne zile aliacha Ukristo wake.
Ukristo na dini za jadi
Kuhusu wanaofuata bado imani asilia pia ni kwamba wanatunza katika mila na desturi zao urithi wa utamaduni. Hata maadili mengine yanayofundishwa kwao yanalingana na sehemu za Biblia. Hakika si vema Wakristo wakiwacheka na kuwaita kwa majina ya dharau kama "Wapagani".
Hata juu ya imani hizo za jadi ni kweli kwamba zilimjua Mungu kwa namna fulani kutokana na uumbaji wake jinsi alivyoandika Mtume Paulo katika Rom 1.
Tazama pia
Ukristo barani Afrika
Ukristo barani Amerika
Ukristo barani Asia
Ukristo barani Australia
Ukristo barani Ulaya
Tanbihi
Neno "Mkristo" (Χριστιανός) lilitumika mara ya kwanza kuhusiana na wafuasi wa Yesu katika
mji
wa Antiokia [Mdo 11:26] mwaka
44
BK
. Wenyewe walikuwa wanajiita "ndugu", "waamini", "wateule", "watakatifu". Katika mazingira ya
Kisemiti
waliendelea na bado wanaendelea kuitwa "Manasara", yaani "Wanazareti" kutokana na jina la
kijiji
alikokulia Yesu. Kumbukumbu ya kwanza ya mwandishi ya neno "Ukristo" (Χριστιανισμός) ni katika barua za
Ignas wa Antiokia
, mwaka
100
hivi. See Elwell/Comfort. Tyndale Bible Dictionary, pp. 266, 828.
Taz. Catholic Encyclopedia (article "Monotheism"); William F. Albright, From the Stone Age to Christianity; H. Richard Niebuhr; About.com, Monotheistic Religion resources; Kirsch, God Against the Gods; Woodhead, An Introduction to Christianity; The Columbia Electronic Encyclopedia Monotheism; The New Dictionary of Cultural Literacy, monotheism; New Dictionary of Theology, Paul, pp. 496–99; Meconi. "Pagan Monotheism in Late Antiquity". p. 111f.
Hinnells,
The Routledge Companion to the Study of Religion
, p. 441.
Zoll, Rachel (Desemba 19, 2011).
"Study: Christian population shifts from Europe"
Associated Press
. Iliwekwa mnamo
25 Februari
2012
{{
cite news
}}
: CS1 maint: date auto-translated (
link
"The Global Religious Landscape: Christianity"
(PDF)
. Pew Research Center. Desemba 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
(PDF)
mnamo 2015-09-24
. Iliwekwa mnamo
2012-07-30
{{
cite web
}}
: CS1 maint: date auto-translated (
link
33.39% of ~7.2
billion world population (under the section 'People')
"World"
. CIA world facts. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2010-01-05
. Iliwekwa mnamo
2015-07-09
{{
cite web
}}
Unknown parameter
ignored (
help
"Christianity 2015: Religious Diversity and Personal Contact"
(PDF)
. gordonconwell.edu. Januari 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
(PDF)
mnamo 2017-05-25
. Iliwekwa mnamo
2015-05-29
{{
cite web
}}
Unknown parameter
ignored (
help
CS1 maint: date auto-translated (
link
"Major Religions Ranked by Size"
. Adherents.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2013-06-22
. Iliwekwa mnamo
2009-05-05
{{
cite web
}}
Unknown parameter
ignored (
help
ANALYSIS (2011-12-19).
"Global Christianity"
. Pewforum.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2018-12-26
. Iliwekwa mnamo
2012-08-17
{{
cite web
}}
Unknown parameter
dead-url=
ignored (
url-status=
suggested) (
help
Martin Luther, Weim., X, P. Il, 107, 8-11
ANALYSIS (2011-12-19).
"Table: Religious Composition by Country, in Percentages"
. Pewforum.org
. Iliwekwa mnamo
2012-08-17
Werner Ustorf. "A missiological postscript", in McLeod and Ustorf (eds),
The Decline of Christendom in (Western) Europe, 1750–2000
, (
Cambridge University Press
, 2003) pp. 219–20.
"The Future of World Religions: Population Growth Projections, 2010-2050"
(PDF)
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
(PDF)
mnamo 2015-05-06
. Iliwekwa mnamo
2017-03-14
Johnstone, Patrick,
"The Future of the Global Church: History, Trends and Possibilities"
, p. 100, fig 4.10 & 4.11
Hillerbrand, Hans J.,
"Encyclopedia of Protestantism: 4-volume Set"
, p. 1815, "Observers carefully comparing all these figures in the total context will have observed the even more startling finding that for the first time ever in the history of Protestantism,
Wider Protestants
will by 2050 have become almost exactly as numerous as Roman Catholics – each with just over 1.5 billion followers, or 17 percent of the world, with Protestants growing considerably faster than Catholics each year."
Marejeo
Albright, William F.
From the Stone Age to Christianity
Alexander, T. Desmond.
New Dictionary of Biblical Theology
Bahnsen, Greg
A Reformed Confession Regarding Hermeneutics
(article 6)
Ilihifadhiwa
4 Desemba 2014 kwenye
Wayback Machine
..
Ball, Bryan; Johnsson, William (ed.).
The Essential Jesus
. Pacific Press (2002).
ISBN 0-8163-1929-4
Barrett, David; Kurian, Tom and others. (ed.).
World Christian Encyclopedia
. Oxford University Press (2001).
Barry, John F.
One Faith, One Lord: A Study of Basic Catholic Belief
. William H. Sadlier (2001).
ISBN 0-8215-2207-8
Benton, John.
Is Christianity True?
Darlington, Eng.: Evangelical Press (1988).
ISBN 0-85234-260-8
Bettenson, Henry
(ed.).
Documents of the Christian Church
. Oxford University Press (1943).
Bokenkotter, Thomas.
A Concise History of the Catholic Church
. Doubleday (2004).
ISBN 0-385-50584-1
Bruce, F.F.
The Canon of Scripture
Chambers, Mortimer; Crew, Herlihy, Rabb, Woloch.
The Western Experience. Volume II: The Early Modern Period
. Alfred A. Knopf (1974).
ISBN 0-394-31734-3
Coffey, John.
Persecution and Toleration in Protestant England 1558–1689
. Pearson Education (2000).
Cross, F. L.; Livingstone, E. A. (ed.).
The Oxford Dictionary of the Christian Church
. Oxford University Press (1997).
ISBN 0-19-211655-X
Deppermann, Klaus.
Melchior Hoffman: Social Unrest and Apocalyptic Vision in the Age of Reformation
ISBN 0-567-08654-2
Dilasser, Maurice.
The Symbols of the Church
. Collegeville, MN: Liturgical Press (1999).
ISBN 0-8146-2538-X
Duffy, Eamon.
Saints and Sinners, a History of the Popes
. Yale University Press (1997).
ISBN 0-300-07332-1
Elwell, Walter A.; Comfort, Philip Wesley.
Tyndale Bible Dictionary
, Tyndale House Publishers (2001).
ISBN 0-8423-7089-7
Esler, Philip F.
The Early Christian World
. Routledge (2004).
Farrar, F.W.
Mercy and Judgment. A Few Last Words On Christian Eschatology With Reference to Dr. Pusey's, "What Is Of Faith?"
. Macmillan, London/New York (1904).
Ferguson, Sinclair; Wright, David, eds. New Dictionary of Theology. consulting ed. Packer, James. Leicester: Inter-Varsity Press (1988).
ISBN 0-85110-636-6
Foutz, Scott.
Martin Luther and Scripture
Ilihifadhiwa
14 Aprili 2000 kwenye
Wayback Machine
Martin Luther and Scripture
Fowler, Jeaneane D.
World Religions: An Introduction for Students
, Sussex Academic Press (1997).
ISBN 1-898723-48-6
Fuller, Reginald H.
The Foundations of New Testament Christology
Scribners (1965).
ISBN 0-684-15532-X
Froehle, Bryan; Gautier, Mary,
Global Catholicism, Portrait of a World Church
, Orbis books; Center for Applied Research in the Apostolate, Georgetown University (2003) ISBN=1-57075-375-X
Funk, Robert.
The Acts of Jesus: What Did Jesus Really Do?
. Polebridge Press (1998).
ISBN 0-06-062978-9
Glenny, W. Edward.
Typology: A Summary Of The Present Evangelical Discussion
Gonzalez, Justo L.
The Story of Christianity: The Early Church to the Dawn of the Reformation
, Harper Collins Publishers, New York (1984).
Hanegraaff, Hank.
Resurrection: The Capstone in the Arch of Christianity
. Thomas Nelson (2000).
ISBN 0-8499-1643-7
Harnack, Adolf von.
History of Dogma
(1894).
Hickman, Hoyt L. and others.
Handbook of the Christian Year
. Abingdon Press (1986).
ISBN 0-687-16575-X
Hinnells, John R.
The Routledge Companion to the Study of Religion
(2005).
Hitchcock, Susan Tyler.
Geography of Religion
National Geographic Society
(2004)
ISBN 0-7922-7313-3
Kelly, J.N.D.
Early Christian Doctrines
Kelly, J.N.D.
The Athanasian Creed
Harper & Row
, New York (1964).
Kirsch, Jonathan.
God Against the Gods
Kreeft, Peter.
Catholic Christianity
. Ignatius Press (2001)
ISBN 0-89870-798-6
Letham, Robert.
The Holy Trinity in Scripture, History, Theology, and Worship
. P & R Publishing (2005).
ISBN 0-87552-000-6
Lorenzen, Thorwald.
Resurrection, Discipleship, Justice: Affirming the Resurrection Jesus Christ Today
. Smyth & Helwys (2003).
ISBN 1-57312-399-4
McLaughlin, R. Emmet,
Caspar Schwenckfeld, reluctant radical: his life to 1540
, New Haven: Yale University Press (1986).
ISBN 0-300-03367-2
MacCulloch, Diarmaid
The Reformation: A History
. Viking Adult (2004).
MacCulloch, Diarmaid,
A History of Christianity: The First Three Thousand Years
. London, Allen Lane. 2009.
ISBN 978-0-7139-9869-6
Marber, Peter.
Money Changes Everything: How Global Prosperity Is Reshaping Our Needs, Values and Lifestyles
. FT Press (2003).
ISBN 0-13-065480-9
Marthaler, Berard.
Introducing the Catechism of the Catholic Church, Traditional Themes and Contemporary Issues
. Paulist Press (1994).
ISBN 0-8091-3495-0
Mathison, Keith.
The Shape of Sola Scriptura
(2001).
McClintock, John,
Cyclopaedia of Biblical, Theological, and Ecclesiastical Literature
. Harper &Brothers, original from
Harvard University
(1889)
McGrath, Alister E
Christianity: An Introduction
. Blackwell Publishing (2006).
ISBN 1-4051-0899-1
McGrath, Alister E.
Historical Theology
McManners, John
Oxford Illustrated History of Christianity
. Oxford University Press (1990).
ISBN 0-19-822928-3
Meconi, David Vincent. "Pagan Monotheism in Late Antiquity", in:
Journal of Early Christian Studies
Metzger, Bruce M., Michael Coogan (ed.).
Oxford Companion to the Bible
Oxford University Press
(1993).
ISBN 0-19-504645-5
Mullin, Robert Bruce.
A short world history of Christianity
. Westminster John Knox Press (2008).
Norman, Edward.
The Roman Catholic Church, An Illustrated History
. University of California (2007)
ISBN 978-0-520-25251-6
Olson, Roger E.,
The Mosaic of Christian Belief
. InterVarsity Press (2002).
ISBN 978-0-8308-2695-7
Orlandis, Jose,
A Short History of the Catholic Church
. Scepter Publishers (1993)
ISBN 1-85182-125-2
Ott, Ludwig.
Grundriß der Dogmatik
. Herder, Freiburg (1965).
Otten, Herman J.
Baal or God? Liberalism or Christianity, Fantasy vs. Truth: Beliefs and Practices of the Churches of the World Today
.... Second ed. New Haven, Mo.: Lutheran News, 1988.
Pelikan, Jaroslav; Hotchkiss, Valerie (ed.)
Creeds and Confessions of Faith in the Christian Tradition
Yale University Press
(2003).
ISBN 0-300-09389-6
Putnam, Robert D.
Democracies in Flux: The Evolution of Social Capital in Contemporary Society
. Oxford University Press (2002).
Riley-Smith, Jonathan.
The Oxford History of the Crusades
. New York: Oxford University Press, (1999).
Robinson, George.
Essential Judaism: A Complete Guide to Beliefs, Customs and Rituals
. New York: Pocket Books (2000).
Schama, Simon .
A History of Britain
. Hyperion (2000).
ISBN 0-7868-6675-6
Servetus, Michael.
Restoration of Christianity
. Lewiston, New York: Edwin Mellen Press (2007).
Simon, Edith.
Great Ages of Man: The Reformation
. Time-Life Books (1966).
ISBN 0-662-27820-8
Smith, J.Z. (1998).
Spitz, Lewis.
The Protestant Reformation
. Concordia Publishing House (2003).
ISBN 0-570-03320-9
Sproul, R.C.
Knowing Scripture
Spurgeon, Charles
A Defense of Calvinism
Ilihifadhiwa
10 Aprili 2008 kwenye
Wayback Machine
Sykes, Stephen; Booty, John; Knight, Jonathan.
The Study of Anglicanism
. Augsburg Fortress Publishers (1998).
ISBN 0-8006-3151-X
Ustorf, Werner. "A missiological postscript", in: McLeod, Hugh; Ustorf, Werner (ed.).
The Decline of Christendom in Western Europe, 1750–2000
. Cambridge University Press (2003).
Walsh, Chad.
Campus Gods on Trial
. Rev. and enl. ed. New York: Macmillan Co., 1962, t.p.
1964. xiv, [4], 154 p.
Woodhead, Linda.
An Introduction to Christianity
Marejeo mengine
Gill, Robin (2001).
The Cambridge companion to Christian ethics
. Cambridge, UK: Cambridge University Press.
ISBN
0-521-77918-9
Gunton, Colin E. (1997).
The Cambridge companion to Christian doctrine
. Cambridge, UK: Cambridge University Press.
ISBN
0-521-47695-X
MacCulloch, Diarmaid.
Christianity: The First Three Thousand Years
(Viking; 2010) 1,161 pages; survey by leading historian
MacMullen, Ramsay (2006).
Voting About God in Early Church Councils
. New Haven, CT: Yale University Press.
ISBN
0-300-11596-2
Padgett, Alan G.; Sally Bruyneel (2003).
Introducing Christianity
. Maryknoll, N.Y.: Orbis Books.
ISBN
1-57075-395-4
{{
cite book
}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (
link
Price, Matthew Arlen; Collins, Michael (1999).
The story of Christianity
. New York: Dorling Kindersley.
ISBN
0-7513-0467-0
{{
cite book
}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (
link
Ratzinger, Joseph
(2004).
Introduction To Christianity (Communio Books)
. San Francisco: Ignatius Press.
ISBN
1-58617-029-5
Roper, J.C.,
Bp
. (1923),
et al.
Faith in God
, in series,
Layman's Library of Practical Religion, Church of England in Canada
, vol. 2. Toronto, Ont.: Musson Book Co.
N.B
.: The series statement is given in the more extended form which appears on the book's front cover.
Tucker, Karen; Wainwright, Geoffrey (2006).
The Oxford history of Christian worship
. Oxford [Oxfordshire]: Oxford University Press.
ISBN
0-19-513886-4
{{
cite book
}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (
link
Wagner, Richard (2004).
Christianity for Dummies
. For Dummies.
ISBN
0-7645-4482-9
Webb, Jeffrey B. (2004).
The Complete Idiot's Guide to Christianity
. Indianapolis, Ind: Alpha Books.
ISBN
1-59257-176-X
Woodhead, Linda (2004).
Christianity: a very short introduction
. Oxford [Oxfordshire]: Oxford University Press.
ISBN
0-19-280322-0
Viungo vya nje
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons
ina media kuhusu:
Christianity
"Christianity"
. Encyclopædia Britannica Online.
"Religion & Ethics—Christianity"
. BBC
. Iliwekwa mnamo
2008-01-03
A number of introductory articles on Christianity.
"Netzarim"
. - Click at 'History Museum' in the left menu
. Iliwekwa mnamo
2008-10-21
The origin of Christianity
Adena, L.
The 'Jesus Cult' and the Roman State in the Third Century
Ilihifadhiwa
4 Januari 2015 kwenye
Wayback Machine
, Clio History Journal, 2008.
Rudishwa kutoka "
Jamii
Makala zinazohitaji uthibitisho
Dini
Ukristo
Yesu Kristo
Dini za Abrahamu
Jamii zilizofichwa:
CS1 maint: date auto-translated
CS1 errors: unsupported parameter
CS1 maint: multiple names: authors list
Pages using ISBN magic links
Ukristo
Weka mada